Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Monday, 9 March 2015

SASA NI ZAMU YA WAKULIMA NA BENKI YA NMB

Benki ya NMB ndio benki pekee yenye matawi katika kila wilaya hapa nchini. Hivyo basi ndio benki pekee inayowajali wateja wake kwa kua karibu zaidi wakati wote. NMB imekua ikiandaa semina elekezi kwa wateja wake. Sasa ilikua zamu ya wakulima na wadau wote wa kilimo cha kahawa wameweza kupata fursa ya kujua huduma mbali mbali zitolewazo na NMB kwa ajili ya wakulima na wadau wote wa huduma za kibenki. Hivi karibuni NMB iliandaa semina kwa ajili ya wadau wa biashara za Kilimo ambayo imeendeshwa katika mikoa mbali mbali ikiwemo Tabora na Mbeya.

Wadau wa kilimo cha kahawa mkoa wa Mbeya wakifuatilia jambo wakati wa semina ya kilimo cha kahawa iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa ajili ya wateja wake ambao ni wadau wa Kilimo Tanzania.
Wadau wa kilimo cha kahawa mkoani Mbeya wakiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za juu baada ya kumaliza semina ya kilimo cha kahawa iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa ajili ya wateja wake ambao ni wadau wa Kilimo Tanzania.

No comments:

Post a Comment