Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Sunday, 15 March 2015

MKAZI WA KOROGWE, TANGA AIBUKA MSHINDI WA MTOKO WA MBUGANI KWENYE FAINALI YA KAMPENI “TUTOKE NA SERENGETI”

Mmoja wa washindi wa shindano la Tutoke na Serengeti, Bw. Godfrey Mpiruka aliyeibuka na zawadi ya Limo Bajaji siku za nyuma akiteta jambo na afisa toka SBL wakati wa kuchezeshwa kwa droo ya mwisho ya shindano hilo, lililofanyika katika baa ya Hongera iliyopo-Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Meneja chapa wa bia ya Serengeti Premium Lager, Bw. Rugambo Rodney (kulia) na msimamizi kutoka PWC, Golder Kamuzora, na Afisa mwandamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha (kushoto), Jehud Ngolo , wakifuatilia kwa karibu namba ya simu ya mshindi wa mwisho wa shindano la Tutoke na Serengeti, ambapo Bw. Robert Gabriel makazi wa Korogwe Tanga aliibuka mshindi.
Meneja chapa wa bia ya Serengeti Premium, Bw. Rugambo Rodney (wa pili kulia), akionyesha namba ya simu ya mshindi wa mwisho wa shindano la Tutoke na Serengeti, ambapo Bw. Robert Gabriel mkazi wa Korogwe, Tanga aliibuka mshindi. Msimamizi toka PWC, Golder Kamuzora (wa tatu kulia), Afisa mwandamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Bw. Jehud Ngolo (wa kwanza kushoto), Afisa Mauzo toka SBL, Anitha Moshi, (wa kwanza kulia). Droo hiyo iliyofanyika katika baa ya Hongera jijini Dar es salaam.


Mmoja wa washiriki wa droo ya mwisho ya “Tutoke na Serengeti,” Morris Maro wa pili toka kulia akibonyeza kitufe cha laptop kuchezesha droo hiyo wakati wa kumtafuta mshindi wa mwisho wa "Mtoko wa mbugani" katika kampeni ya Tutoke na Serengeti. Droo hiyo ilifanyika Hongera baa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es salaam amapo Bw. Robert Gabriel mkazi wa Korogwe, Tanga aliibuka mshindi. Kwenye picha ni Meneja chapa wa bia ya Serengeti premium Bw. Rugambo Rodney (wa pili kushoto), Afisa mwandamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Jehud Ngolo (wa kwanza kushoto), na Getrud Mzava, mteja aliyeitwa kushuhudia, droo hiyo ikichezeshwa kwa haki ndani ya ukumbi wa Hongera baa-Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Mmoja wa wateja wa Serengeti Premium Lager, Getrud Mzava, akitaja namba za simu za mshindi wa mwisho katika droo ya Tutoke na Serengeti wakati wa kumtafuta mshindi wa mwisho wa Mtoko wa mbugani, ambapo mkazi wa Korogwe, Tanga, Bw. Robert Gabriel aliibuka mshindi wa Mtoko wa Mbugani. Droo hiyo ilichezeshwa ndani ya ukumbi wa Hongera-Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Meneja chapa wa bia ya Serengeti Premium Lager, Bw. Rugambo Rodney, (wa pili kushoto) akiongea kwa njia ya simu na mshindi wa mtoko wa mbugani, Bw. Robert Gabriel mkazi wa Korogwe-Tanga, baada ya kuibuka mshindi wa mwisho wa shindano la Tutoke na Serengeti katika droo iliyochezeshwa ndani ya ukumbi wa Hongera baa-Kijitonyama jijini Dar es salaam. Kushoto ni Afisa mwandamizi toka Bodi ya michezo ya kubahatisha, Jehud Ngolo.
Meneja chapa wa bia ya Serengeti Premium Bw. Rugambo Rodney, (kushoto) akiongea kwa njia ya Simu na mshindi wa "Mtoko wa mbugani" Robert Gabriel mkazi wa Korogwe-Tanga, baada ya kuibuka mshindi wa mwisho wa shindano la Tutoke na Serengeti. Droo hiyo ilichezeshwa ndani ya ukumbi wa Hongera Baa-Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Wasanii toka SBL wakikonga nyoyo za washiriki wa Droo ya Tutoke na Serengeti wakati wa kumtafuta mshindi wa mwisho wa “Mtoko wa Mbugani” ambapoBw.Robert Gabriel toka Korogwe-Tanga aliibuka mshindi wa droo hiyo iliyochezeshwa jana katika Baa ya Hongera iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
12/03/2015, Dar es Salaam: Droo ya mwisho ya kampeni ya Tutoke na Serengeti imemshuhudia mkazi wa Korogwe Tanga Bw. Robert Gabriel Moriale akitangazwa mshindi katika fainali ya kampeni “Tutoke na Serengeti”. Fainali hiyo imefanyika katika ukumbi wa Baa ya Hongera iliyopo maeneo ya Kijitonyama-Dar es salaam karibu na chuo cha Ustawi wa jamii.

Mshindi huyo alijipatia fursa ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambapo ataongozana na mtu wake yeyote wa karibu kwa muda wa siku tatu huku SBL kupitia bia yake ya Serengeti Premium ndio itahusika kugharamia usafiri, chakula, malazi sambamba na fedha taslim za mshindi kujikimu pindi atakapokua safarini.

Akiongea kupitia njia ya simu mara baada ya kutangazwa mshindi wa mtoko wa mbugani, Bw.Robert (49)alipokea taarifa hizo kwa furaha na alisikika akishangilia kwa kelele baada ya kuambiwa kwamba amejishindia “Mtoko wa Mbugani”.

Alipoulizwa kama alishawahi kushinda chochote kabla ya zawadi hiyo, Robert alijibu “Nimekuwa nikishiriki tangu mwanzo na nimepata bia za bure nyingi tu pamoja na pungozo la Tsh 300. Lakini hii ya leo kwa kweli sikuitarajia kabisa”

Akiongea wakati wa kufunga kampeni hiyo, Meneja chapa wa bia ya Serengeti Premium Lager , Bwana Rugambo Rodney alisema, “Tumefurahishwa sana na ushindi wa bwana Robert na tunapenda kumshukuru kwa kushiriki na tunaamini aliifurahia bia ya Serengeti Premium ambayo imemletea furaha ya kipekee siku ya leo.

Rodney pia alitumia fursa hiyo kuwashukuru washiriki wote kwa kutumia muda wao wa thamani katika promosheni hii na kuwapa moyo wale ambao hawakubahatika kushinda mtoko wa mbugani, Bajaj au bia za bure kutokata tamaa na kushiriki tena nyakati zijazo kwani SBL imekuwa mstari wa mbele katika kurudisha kiasi cha faida waliyopata kwa wateja wake. Aliongeza kuwa wateja wakae mkao wa kula kwani kuna kitu kikubwa kinaandaliwa kwa ajili yao.

Wakati kampeni hii iliyodumu takribani miezi minne inafikia tamati, SBL imetoa shukrani za pekee kwa wateja wake wa Serengeti Premium Lager baada ya kushuhudia washiriki zaidi ya milioni moja wakijaribu bahati zao na kuifanya promosheni ya “Tutoke na Serengeti” kuwa yenye mafanikio kutokana na muitikio mkubwa na uelewa kutoka kwa wananchi.


Kampeni imewazawadia wateja mbalimbali fursa ya kutembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti wakati wengine wakiondoka na zawadi murua kama vile Limo Bajaj ambazo kwa kiasi kikubwa zitabadilisha maisha yao. Kulikuwa pia na fedha taslim za kila wiki, bia za bure, na punguzo la Tshs300 katika kila bia ya Serengeti Premium.

Promosheni hii ya nchi nzima pia ilipata ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa B-Pesa, wataalamu wa teknolojia mpya ya usambazaji fedha waliochangia Limo Bajaj sita kwa washindi mbalimbali. Pia walihusika na usambazaji wa fedha kwa washindi nchi nzima katika kipindi chote cha miezi mine ya kampeni.

No comments:

Post a Comment