Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 30 September 2014

VODACOM NA BENKI YA TWIGA BANCORP ZAWALETEA HUDUMA YA "M-PESA SUPER AGENCY"

Mwenyekiti wa bodi ya benki ya Twiga Bancorp Prof. Amon Mbelle (wapili toka kulia) akipongezana na Mkuu wa Mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya Pwani, Herieth Koka, mara baada ya kuzinduliwa kwa huduma ya ”M-PESA SUPER AGENCY” itakayowawezesha wateja wa benki hiyo kupata huduma za kifedha kiurahisi kupitia simu za mkononi. Kushoto ni Kaimu Ofisa mkuu wa Benki hiyo Willace Msemo na Meneja uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia).

Mkuu wa Mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya Pwani, Herieth Koka (kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na huduma ya ”M-PESA SUPER AGENCY” itakayowawezesha wateja wa benki ya Twiga Bancorp kupata huduma za kifedha kiurahisi kupitia simu za mkononi. katikati ni Mwenyekiti wa bodi wa benki hiyo Prof. Amon Mbelle na kushoto ni Meneja uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu.

No comments:

Post a Comment