Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 17 September 2014

RAIS KIKWETE ZIARANI NCHINI MAREKANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini usiku wa Jumatatu, Septemba 15, 2014, kuanza ziara ya wiki mbili katika Marekani ambapo atahutubia Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) New York.

Mbali na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Kikwete pia atahudhuria mikutano muhimu katika mji mkuu wa Marekani, Washington, D.C.

Mjini New York, Rais Kikwete atashiriki katika mikutano mikubwa zaidi ya 10 ikiwa ni pamoja na kuhutubia Baraza Kuu wakati wa Majadiliano ya Jumla ( General Debate) yaliyopangwa kufanyika Septemba 24 hadi 27 na Septemba 29 hadi Oktoba Mosi, mwaka huu, 2014.


Rais Kikwete amepangwa kuwa kiongozi wa 12 duniani kuhutubia Baraza hilo mchana wa Alhamisi ijayo, Septemba 25, 2014. Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utaanza Septemba 16 hadi Desemba 24, mwaka huu, Miongoni mwa mikutano mingine muhimu ambayo Rais Kikwete atashiriki ni pamoja na kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) Kuhusu Mazingira (CAHOSC) na Mkutano wa Wakuu wa Nchi Kuhusu Mazingira ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Mheshimiwa Ban Ki Moon.


Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam. 
16 Septemba , 2014.

No comments:

Post a Comment