Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 24 September 2014

MRADI WA NYUMBA WA DEGE ECO-VILLAGE WAANZA

Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Bw. Azhar Malik akifafanua juu ya mradi huo wa Dege Eco-Village kwa wateja wapitao kwenye banda lao (hawapo pichani).

Mradi wa nyumba unaosimamiwa na kampuni ya Hifadhi inayoitwa Dege Eco-Village umeshiriki maonyesho ya nyumba yaliyoanza kufanyika jijini Dar es Salaam jumatatu.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege Eco-Village alisema “Kwa sasa ujenzi unaendelea na karibu aina ya nyumba (apartment) 3,000 zitakuwa tayari ifikapo Januari 2015. Aliongezea kusema kwamba kupitia mradi huu waTanzania watanufaika kwa kupata ajira na pia kuwa na huduma kama hospitali, shule na maduka katika eneo la Kigamboni.

Mradi huu unajengwa kwenye eneo takriban eka 300 na kampuni hiyo imewekeza zaidi ya dola milioni 350. Kwa ujumla nyumba aina ya villa ziko 300 na apartment ziko 7,400. Mradi huu utakamilika mwaka 2018. Apartment zitakamilika mwaka 2017 na villa mwaka 2018.

Ndani ya mji huu wa Dege Eco-Village wakazi hawatahitaji kwenda popote kwasababu kila kitu kitakuwepo kama shule za watoto, kituo cha polisi, hospitali, supermarket na kadhalika.

Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Bw. Azhar Malik akihojiwa na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika maonyesho ya nyumba.

 Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Bw. Azhar Malik (katikati) akiongea na mteja kuhusu mradi huo wa Dege Eco-Vilage. Kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi wa Masoko na Mauzo, Bw. Adam Jusab.

Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Bw. Azhar Malik akiwa na wateja ambao wametembelea banda hilo na kuwaonyesha vifurushi vya mradi huo.

No comments:

Post a Comment