Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 5 August 2014

MKUU WA MKOA WA PWANI AZINDUA MRADI MPYA WA VIWANJA VYA PANGANI, KIBAHA

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mh. Mwantumu Mahiza akikata Utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi mpya wa Viwanja vya Pangani Mjini Kibaha, Mkoani Pwani jana Agosti 4, 2014. Mradi huo Unaratibiwa na Kampuni ya Space & Development kwa Ufadhili wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB Development Bank).

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mh. Mwantumu Mahiza akiangalia maji yanayotoka kwenye Kisima kikubwa kilichopo ndani ya mradi huo ambacho kina uwezo wa kutoa lita elfu 10 kwa saa, ikiwa ni sehemu ya miundombinu iliyopo ndani ya mradi huo.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mh. Mwantumu Mahiza akizungumza na baadhi ya wadau (hawapo pichani) waliohudhuria kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa Mradi mpya wa Viwanja vya Pangani Mjini Kibaha, Mkoani Pwani jana Agosti 4, 2014. Mradi huo Unaratibiwa na Kampuni ya Space & Development kwa Ufadhili wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB Development Bank).

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimani nchini (TIB Development Bank), Peter Noni akizungumza machache juu ya namna walivyojitokeza kusaidia kuufanikisha mradi huo ikiwa ni pamoja na kusaidia maendeleo ya maeneo mbali mbali ndani ya Mkoa wa Pwani, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi mpya wa Viwanja vya Pangani Mjini Kibaha, Mkoani Pwani jana Agosti 4, 2014. 

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Space & Development, Renny Chiwa akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika eneo la Pangani, Kibaha Mkoani Pwani.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mh. Mwantumu Mahiza akipongezana na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimani nchini (TIB Development Bank), Peter Noni mara baada ya hotuba yake.

Picha ya pamoja.


Source: Michuzi Blog

No comments:

Post a Comment