Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Absa Banner_211026

Stanbic Bank Banner_201026

Thursday, 23 January 2025

SERIKALI KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI KATIKA MICHEZO YA KUBAHATISHA NCHINI

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania GBT, Mhe. Balozi Modest Mero (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Bw. James Mbalwe (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Kampuni ya Ithuba Tanzania, Bw. Kelvin Koka (wa kwanza kushoto), na Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Ithuba Afrika, Bw. Mpange Chapeshamano, kabla ya kufanyika kwa hafla ya kuitambulisha Kampuni ya ITHUBA kama mwendeshaji wa Bahati Nasibu ya Taifa baada ya kuibuka mshindi katika mchakato wa zabuni ulioendeshwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akizungumza jambo wakati wa hafla ya kuitambulisha Kampuni ya ITHUBA kama mwendeshaji wa Bahati Nasibu ya Taifa baada ya kuibuka mshindi katika mchakato wa zabuni ulioendeshwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), katika Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (kulia), akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania GBT, Mhe. Balozi Modest Mero wakati wa hafla ya kuitambulisha Kampuni ya ITHUBA kama mwendeshaji wa Bahati Nasibu ya Taifa.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania GBT, Mhe. Balozi Modest Mero (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Bw. James Mbalwe (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Kampuni ya ITHUBA Tanzania, Bw. Kelvin Koka (wa pili kulia), na Mkuu wa Masoko na Masuala ya Kampuni wa ITHUBA Afrika, Bi. Michelle Van Trotsenburg (wa kwanza kulia), wakifuatilia maswali ya wanahabari wakati wa hafla ya kutambulisha Kampuni ya ITHUBA kama mwendeshaji wa Bahati Nasibu ya Taifa.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (katikati mstari wa mbele), Mwenyekiti wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania GBT, Mhe. Balozi Modest Mero (wa nne kushoto), Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Bw. James Mbalwe (wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa Kampuni ya ITHUBA Tanzania, Bw. Kelvin Koka (wa nne kulia), Mkuu wa Masoko na Masuala ya Kampuni wa ITHUBA Afrika, Bi. Michelle Van Trotsenburg (wa tatu), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha, Bodi ya GBT na Kampuni ya ITHUBA, baada ya kumalizika kwa hafla ya kuitambulisha Kampuni ya ITHUBA kama mwendeshaji wa Bahati Nasibu ya Taifa baada.

Serikali imeahidi kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji katika michezo ya kubahatisha nchini kwa kuwa ni moja ya chanzo muhimu cha mapato ya kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), wakati wa hafla ya kutambulisha Kampuni ya ITHUBA kama mwendeshaji wa Bahati Nasibu ya Taifa baada ya kuibuka mshindi katika mchakato wa zabuni ulioendeshwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT).

Mhe. Chande alisema kuwa, Serikali inajivunia hatua ilizochukua kufanikisha mradi huo mkubwa wa mabadiliko ya Bahati Nasibu ya Taifa ambayo ni ishara ya matumaini, fursa na maendeleo, ambapo kila tiketi ya Bahati Nasibu inayonunuliwa, mbali na nafasi ya kushinda, ni mchango kwa maendeleo ya Taifa letu.

Aliongeza kuwa uteuzi wa Kampuni ya ITHUBA Tanzania kama mwendeshaji rasmi wa Bahati Nasibu ya Taifa unaonesha uwezo wao wa hali ya juu na uelewa wa kina wa mahitaji ya Tanzania na uteuzi huo ulizingatia utaalam na uzoefu wa ITHUBA, kama mwekezaji wa kimataifa mwenye rekodi nzuri ya kuendesha biashara ya Bahati Nasibu za Taifa barani Afrika ambako inaendesha michezo hiyo katika nchi ya Afrika ya Kusini, Uganda na nyinginezo.

“Ni imani yangu kuwa ITHUBA imejipanga vyema ili Bahati Nasibu ya Taifa iweze kuendeshwa kwa ufanisi na kuleta mafanikio yaliyotarajiwa na hatua hii inafungua matarajio makubwa katika ufanisi wa uendeshaji wa Bahati Nasibu ya Taifa na ukurasa mpya wa mabadiliko katika sekta ya michezo ya kubahatisha hapa nchini Tanzania” alisema Mhe. Chande.

NOTI MPYA KUANZA KUTUMIKA TAREHE 1 FEBRUARI 2025

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akipokea Noti Mpya kifani za shilingi elfu kumi, elfu Tano, elfu Mbili na shilingi elfu moja, kutoka kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, Noti ambazo zitaanza kutumika sambamba na Noti zilizopo hivi sasa, kuanzia tarehe Mosi Februari, 2025.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emanuel Tutuba amesema kuwa Noti Mpya za Tanzania zenye Saini ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na yeye mwenyewe, za toleo la mwaka 2010, zitaingia kwenye mzunguko kuanzia tarehe mosi Februari mwaka huu.

Gavana Tutuba amesema hayo wakati akimkabidhi Mhe. Dkt. Nchemba, Noti kifani za shilingi elfu kumi, elfu Tano, Elfu Mbili na Shilingi Elfu moja, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zinazosimamia masuala ya fedha nchini.


“Mheshimiwa Waziri, ninayo furaha kukujulisha kuwa zoezi letu la uchapaji upya wa Noti kwa marejeo ya toleo la mwaka 2010, limekamilika na tayari tumewajulisha wananchi kupitia taarifa niliyoitoa kupitia Gazeti la Serikali” alisema Bw. Tutuba.

Gavana Tutuba alifafanua kuwa Noti hizo zitatumika sambamba na Noti zilizopo hivi sasa, zinamwonekano wa Noti zinazotumika hivi sasa zilizotolewa Mwaka 2010, ikiwemo alama za usalama, ukubwa, rangi na mambo mengine, isipokuwa ina marekebisho kwenye saini ya Waziri wa Fedha, na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.


“Saini ya aliyekuwa Waziri wa Fedha ambaye hivi sasa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango imebadilishwa na kuwekwa Saini yako Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Saini ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania aliyestaafu, Prof. Florens Luoga, imebadilishwa na kuwekwa Saini ya Gavana wa Benki Kuu wa sasa, Bw. Emmanuel Tutuba” aliongeza Bw. Tutuba.

DAR ES SALAAM WINE WEEK FESTIVAL; SAVE THE DATE - FEBRUARY 1, 2025



BENKI YA STANBIC YAZINDUA KAMPENI YA MALIPO YA KIDIGITALI "TAP KIBINGWA"

Akizungumza kutoka makao makuu ya Benki ya Stanbic jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Benki Binafsi na ya Watu Binafsi - Omari Mtiga (katikati), alisema kuwa mpango huu unaonyesha dhamira ya benki katika ubunifu, uwezeshaji wa wateja, na ukuaji endelevu.  
Akizungumza kutoka makao makuu ya Benki ya Stanbic jijini Dar es Salaam, Meneja wa Kitengo cha Kutoa Kadi - Irene Mutabihirwa (wa pili kulia) alizindua kampeni ya Visa Debit Card inayoitwa 'Tap Kibingwa.'
Mkurugenzi wa Wateja na Huduma Binafsi - Omari Mtiga (kulia), Meneja wa Kitengo cha Kutoa Kadi - Irene Mutabihirwa (kushoto), na dereva maarufu wa mbio za magari Tanzania - Dharam Pandya (katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja inayoonesha moja ya zawadi ya mshindi wa kwanza wa droo ya "Tap Kibingwa na Kadi ya Visa ya Stanbic benki" Suzuki Fronx. 
  • Benki ya Stanbic Tanzania yazindua kampeni ya “Tap Kibingwa” ili kuhamasisha malipo ya kidigitali kupitia Kadi za Visa Debit
  • Wateja wanapata nafasi ya kushinda zawadi za kuvutia, ikiwa ni pamoja na zawadi za fedha za TZS 300,000 na TZS 500,000 kila mwezi, na zawadi kuu ya gari jipya aina ya Suzuki Fronx na mapumziko ya kifahari ya siku tatu Zanzibar
  • Kampeni inalenga kukuza matumizi ya malipo kupitia mashine za POS na eCommerce kwa ajili ya uzoefu wa usalama, urahisi, na manufaa
Dar es Salaam, Januari 15, 2025: Benki ya Stanbic Tanzania imezindua rasmi mpango wake mpya, kampeni ya “Tap Kibingwa,” iliyoundwa ili kukuza suluhisho za malipo ya kidigitali na kuwazawadia wateja wake. Kampeni hii itakayoendeshwa kuanzia Januari 10 hadi Machi 31, 2025, inawahamasisha wateja kutumia Kadi zao za Visa Debit kwa miamala ya POS na eCommerce ili kushinda zawadi za kuvutia.


Akizungumza wakati wa uzinduzi, Omari Mtiga, Mkurugenzi wa Wateja na Huduma Binafsi wa Benki ya Stanbic, alielezea malengo ya kampeni: “Katika Stanbic, tumejizatiti kukuza mtindo wa maisha wenye usalama, urahisi, na zawadi kwa wateja wetu. Kampeni ya ‘Tap Kibingwa’ inaakisi dhamira hii, kwa lengo la kuwawezesha Watanzania kupitia miamala rahisi ya kidigitali huku tukiwapa zawadi za kuvutia. Tunakaribisha kila mtu kushiriki nasi katika safari hii ya uwezeshaji wa kifedha.”


Muundo wa Zawadi unajumuisha:
  • Zawadi za Kila Mwezi: Wateja watakaotumia TZS 2,000,000 au zaidi kwa mwezi wataingia kwenye droo ya kushinda TZS 300,000, huku wale wanaotumia TZS 5,000,000 au zaidi wataingia kwenye droo ya kushinda TZS 500,000.
  • Droo Kuu: Wateja watakaofanya miamala angalau 50 yenye thamani ya TZS 30,000,000 au zaidi ndani ya kipindi cha kampeni watahitimu kushiriki droo kuu kushinda gari jipya aina ya Suzuki Fronx na mapumziko ya kifahari ya siku tatu Zanzibar kwa wawili.
Irene Mutabihirwa, Meneja wa Kitengo cha Kutoa Kadi wa Benki ya Stanbic, alisisitiza kuhusu zawadi: “Kampeni hii haihusu tu miamala. Ni kuhusu kuwathamini wateja wetu na kuwapa nafasi ya kushinda zawadi za kuvutia. Kuanzia zawadi za fedha hadi zawadi kuu ya gari jipya aina ya Suzuki Fronx na mapumziko Zanzibar, tunafurahia kusherehekea wale wanaokubali malipo ya kidigitali pamoja nasi.”

Wednesday, 22 January 2025

ABSA BANK CONCLUDES SPEND & WIN CAMPAIGN WITH GREAT SUCCESS

The final winner of Absa Bank 3-month Spend & Win campaign, Ms. Amalia Lui Shio (center), receives an ignition key to a brand-new 2024 Subaru Forester from the bank’s Head of Retail Banking, Ms. Ndabu Lilian Swere, during a ceremony held in Dar es Salaam. The campaign aimed to encourage more customers to adopt digital banking solutions, such as debit and credit cards, which offer safety, convenience, and access to a wide range of banking services. Also present were senior officials from Absa Bank.
The final winner of Absa Bank 3-month Spend & Win campaign, Ms. Amalia Lui Shio (center), dances alongside traditional ngoma artists during the handover ceremony of a brand-new 2024 Subaru Forester. The vehicle was presented to her by the bank’s Head of Retail Banking, Ms. Ndabu Lilian Swere, in Dar es Salaam.
The final winner of Absa Bank 3-month Spend & Win campaign, Ms. Amalia Lui Shio, in a jovial mood shortly after receiving her brand-new 2024 Subaru Forester from the bank’s Head of Retail Banking, Ms. Ndabu Lilian Swere, during a ceremony held in Dar es Salaam.
Absa Bank staff celebrate with Ms. Amalia Lui Shio, the final winner of the bank’s 3-month Spend & Win campaign, shortly after she received her brand-new 2024 Subaru Forester during a ceremony held in Dar es Salaam.
Ms. Amalia Lui Shio, the final winner of the Absa Bank Spend & Win 3-month campaign, drives off in her brand-new 2024 Subaru Forester shortly after receiving it at a function held in Dar es Salaam.

HYATT REGENCY NAIROBI WESTLANDS SET TO BOOST KENYA'S ECONOMY & TOURISM



Nairobi, Kenya; 22nd January 2025: In a significant advancement for Kenya’s hospitality sector and economy, Hyatt Hotels Corporation officially unveiled its first hotel in the country, the Hyatt Regency Nairobi Westlands, on January 22, 2025. Located in the vibrant Westlands neighborhood, this five-star hotel is poised to enhance not only tourism but also business opportunities in the region, thereby reinforcing Nairobi’s status as a premier destination for both leisure and corporate travel.

The Hyatt Regency Nairobi Westlands, featuring 219 rooms, stands strategically in one of Nairobi’s foremost commercial and tourist hubs. The hotel aims to cater to the burgeoning demand from business travelers and tourists alike, positioning itself as a prime venue for meetings and events. With an array of amenities and a focus on delivering a distinctive hospitality experience that marries local cultural elements with Hyatt's renowned service standards, the hotel is anticipated to draw additional inbound tourism while supporting the local economy.

Stephen Ansell, Managing Director for Middle East and Africa at Hyatt, expressed enthusiasm over the hotel’s launch, noting, “This debut signifies a substantial milestone in Hyatt's African growth strategy. We are dedicated to expanding into desirable destinations, ensuring the diverse needs of modern travelers are met, as we offer our World of Hyatt members and customers enhanced choices.” This expansion underscores Kenya’s increasing attractiveness as an international travel destination.

SHOWMAX ORIGINAL DRAMA JACOB'S DAUGHTERS PREMIERES ON 23 JAN. 2025



Showmax continues to bring the best in original African storytelling with Jacob's Daughters, a gripping Tanzanian family drama filled with love, betrayal, and unbreakable bonds. The 13-part series premieres on 23 January 2025, with new episodes on Thursdays.

At the heart of Jacob's Daughters is a tale of four half-sisters: Nuru (played by Wisher Nakamba), Nana (played by Angel Mazanda), Caroline (played by Prisca Lyimo) and Candy (played by Sia Tarimo). They are brought together by their father, Mr Jacob (played by Cojack Chilo), but divided by decades of drama. The sisters are pulled into an emotional whirlwind of romantic entanglements, secrets, and struggles against their father's complicated relationships.

As conflicts intensify, the sisters find their unity tested when Mr Jacob falls for Diana (played by Ahlam Khamis Salum), a charismatically divisive figure. Diana's presence threatens not only their family bond but also the family's stability, forcing the sisters to confront their past and fight for their future.

Created by Leah Mwendamseke aka Lamata, the award-winning storyteller and director behind Big Surprise and Inside, Jacob's Daughters promises to captivate viewers with its emotional depth, richly drawn characters, and relatable themes of love, loyalty, and resilience.

DSE MARKET CAPITALIZATION SEES STRONG GROWTH IN 2024

DSE STRENGTHENS COLLABORATION FOR A THRIVING FINANCIAL SECTOR

Peter Nalitolela, CEO of Dar es Salaam Stock Exchange - DSE (left), and the Executive Director of Tanzania Institute Of Bankers (TIOB), Patrick Mususa (right) have signed a landmark Memorandum of Understanding (MoU), fostering greater cooperation in financial market development, capacity building, and professional growth in Tanzania's banking and securities sectors.

Tuesday, 21 January 2025

VODACOM YAHITIMISHA KAMPENI YA "SHANGWE POPOTE UKIWA NA M-PESA"

Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania Plc Mkoa wa Pwani, Suleiman Amri (katikati) akiweka mafuta yaliyotolewa bure kwa wateja wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam kwenye gari ya Ramadhan Kalafya (kushoto) ikiwa ni mwisho wa kampeni yao ya kurudisha tabasamu kwa wateja katika msimu wa sikukuu inayoitwa ‘Shangwe popote ukiwa na M-Pesa'.
Msimamizi wa Mauzo kutoka Vodacom Tanzania Plc Mkoa wa Dar es Salaam, Neema Lucas (katikati) akiweka mafuta yaliyotolewa bure kwa wateja wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam kwenye gari ya John John (kushoto) ikiwa ni mwisho wa kampeni yao ya kurudisha tabasamu kwa wateja katika msimu wa sikukuu inayoitwa ‘Shangwe popote ukiwa na M-Pesa'.
Msimamizi Mauzo kutoka Vodacom Tanzania Plc Mkoa wa Dar es Salaam, Nakiete Mshana (kulia) akiweka mafuta yaliyotolewa bure kwa wateja wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam kwenye gari ya Beatrice Msofero (katikati) ikiwa ni mwisho wa kampeni yao ya kurudisha tabasamu kwa wateja katika msimu wa sikukuu inayoitwa ‘Shangwe popote ukiwa na M-Pesa'.
Msimamizi wa Mauzo kutoka Vodacom Tanzania Plc Mkoa wa Dar es Salaam, Mishi Bakari (kulia) akiweka mafuta yaliyotolewa bure kwa wateja wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam kwenye pikipiki ya Daud Neto (katikati) ikiwa ni mwisho wa kampeni yao ya kurudisha tabasamu kwa wateja katika msimu wa sikukuu inayoitwa ‘Shangwe popote ukiwa na M-Pesa'.

SOUTH AFRICAN AIRWAYS RELAUNCHES DAILY FLIGHTS TO DAR ES SALAAM



Johannesburg / Dar es Salaam, 16 January 2025: The countdown is on at South African Airways (SAA) to relaunch daily flights between Johannesburg and Dar es Salaam in Tanzania.

“This flight is not simply a milestone for SAA and linking Johannesburg and Dar es Salaam through air travel; it heralds a bridge that connects two of Africa’s most influential economies and strengthens the friendship between our nations”, says SAA’s interim CEO, Professor John Lamola.

“It brings together industries, communities and resources, enabling us to unlock greater prosperity, foster collaboration and generate new opportunities for trade, investment and development for both our economies, and for the people of South Africa and Tanzania.”


Broader economic growth

Dar es Salaam is East Africa’s largest city by population size and is an important regional economic and logistical hub. It is also a gateway for popular tourist attractions in the region.

South Africa accounts for a significant proportion of foreign direct investment in Tanzania, and the two countries have a robust trade in agricultural products, precious metals, chemicals and machinery.

Lamola said the relaunch represents SAA’s strategic initiative to strengthen the airline’s presence across Africa.

“SAA’s regional network has emerged as a top performer, contributing significantly to the revenue of the SAA Group. More importantly, these regional connections are crucial for the broader economic growth of South Africa,” he said.

Flight schedule

Daily flights will depart OR Tambo International Airport in Johannesburg at 10pm (SAST) and arrive at Julius Nyerere International Airport in Dar es Salaam at 2.30am (EAT). The daily service from Dar es Salaam to Johannesburg will depart at 5.10am (EAT) to arrive in Johannesburg at 7.55am (SAST). Dar es Salaam is one hour ahead of Johannesburg.

Lamola said the schedule of seven weekly return flights has been engineered to accommodate both point-to-point and connecting passengers.

Consolidating SAA’s regional network

In November last year, SAA expanded its services to Harare (Zimbabwe) and Lusaka (Zambia) to 12 flights per week, up from 10 and seven flights a week, respectively. Flights to Lagos (Nigeria) and Accra (Ghana) have been increased from three to four times a week, while SAA is flying to Kinshasa in the Democratic Republic of Congo (DRC) five times a week. SAA also began flying to the DRC’s mining hub, Lubumbashi, in November.

VODACOM YATAJWA MWAJIRI BORA TANZANIA KWA MWAKA WA NANE MFULULIZO

  • Nambari 1 Mwajiri Bora Tanzania kwa mwaka 2025
16 Januari 2024, Dar es Salaam: Kwa mwaka wa nane mfululizo, kampuni ya Vodacom Tanzania PLC imethibitishwa kuwa Mwajiri Bora na Taasisi ya Waajiri Bora (Top Employer Institution) huku ikishika nafasi ya kwanza nchini kwa mwaka 2025. Utambuzi huu wa heshima na nafasi ya kwanza miongoni mwa Waajiri Bora waliothibitishwa pia imetolewa kwa kundi la Makampuni ya Vodacom barani Afrika (Vodacom Group), Vodacom Afrika Kusini, Vodacom Msumbiji na Safaricom Kenya.

Mwaka 2024, Vodacom iliboresha programu yake ya kuongeza thamani kwa Wafanyakazi wake kwa kuongeza huduma zinazothibitisha adhma yake ya kuunda mazingira ya kazi jumuishi. Kwa kutilia mkazo mafunzo na maendeleo ya ujuzi, ushirikishwaji wa wafanyakazi, sera thabiti za likizo na utamaduni mzuri wa kazi, Vodacom imeendelea kuonesha njia katika nyanja ya mahusiano ya wafanyakazi nchini.

“Kudumisha nafasi yetu kama Mwajiri Bora hapa nchini, kunadhihirisha ari yetu ya kuwawezesha wafanyakazi wetu kufanya kazi kwa bidii. Tumeweka kipaumbele kwenye kuwafanya wafanyakazi wetu wajisikie kuthaminiwa kwa kutoa faida mbalimbali kwao na familia zao, kukuza vipaji vya vijana kupitia mpango wetu wa mafunzo ya Wahitimu (Graduate Trainee) miongoni mwa mipango mingine, kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika teknolojia kupitia programu yetu ya Code Like a Girl kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 – 18 na hivi karibuni, tulianzisha Kituo cha kuongeza ujuzi wa Kidigitali kinachotoa mafunzo kwa njia ya mtandao kwa vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 ambao ni mustakabali wa kazi katika uchumi wa kidigitali unaokua kwa kasi,” anasema Vivienne Penessis, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa kampuni hiyo.

Monday, 20 January 2025

BENKI YA CRDB YASHINDA TUZO MBILI ZA KIMATAIFA ZA MWAJIRI BORA "TOP EMPLOYER"


Dar es Salaam, Januari 20, 2025: Benki ya CRDB imeendelea kung’ara kimataifa baada ya kutunukiwa tuzo 2 za Mwajiri Bora (Top Employer) na taasisi ya kimataifa ya Top Employers Institute. Ushindi huu unaiweka Benki ya CRDB katika nafasi ya kipekee kama moja ya waajiri bora barani Afrika, ikitambua jitihada zake za kujenga mazingira bora ya kazi yanayochochea ubunifu, ustawi wa wafanyakazi, na maendeleo ya kitaaluma.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Godfrey Rutasingwa, alisema tuzo hizo zinadhihirisha juhudi za dhati za kuboresha maisha ya wafanyakazi wake ndani na nje ya kazi.


“Tuzo hii ni ishara ya wazi kwamba Benki ya CRDB inajali na kuthamini wafanyakazi wake, ikiwapa mazingira bora yanayowezesha mafanikio yao binafsi na ya kitaaluma. Huu ni ushindi wa pamoja, si wa benki pekee bali pia ni wa familia nzima ikiwamo wateja na wadau wote wa Benki ya CRDB,” amesema.

Tuzo ya Top Employer inatolewa baada ya tathmini ya kina ya viwango vya usimamizi wa rasilimali watu, ikiwa ni pamoja na uwekezaji katika maendeleo ya kitaaluma, usawa wa kijinsia, programu za afya na ustawi wa wafanyakazi, na utamaduni wa uwazi na mshikamano. Katika maeneo haya, Benki ya CRDB imeonyesha ubora wa kipekee, ikiwasaidia wafanyakazi wake kufanikisha ndoto zao za kitaaluma huku wakichangia ukuaji wa Benki hiyo kwa kasi.



Tuzo za Top Employer ni mwendelezo wa Benki ya CRDB kutambuliwa kimataifa ambapo katika mwaka 2024 pekee, Benki hiyo ilikusanya tuzo zaidi ya 50 za kimataifa, ikiwa ni pamoja na Benki Bora Tanzania, huduma bora kwa wateja, ubora wa huduma za kidijitali, na ufanisi wa mikakati ya maendeleo endelevu. Tuzo ya Top Employer ni nyongeza ya heshima inayodhihirisha dhamira ya benki hiyo ya kuimarisha rasilimali watu kama msingi wa mafanikio yake.

Rutasingwa alibainisha kuwa Benki ya CRDB inajipanga kuimarisha nafasi yake kama kinara wa usimamizi wa vipaji barani Afrika. “Tunajivunia kuwa sehemu ya mabadiliko yanayoangazia wafanyakazi kama rasilimali muhimu. Maendeleo endelevu ya benki yetu hayawezekani bila jitihada za kila mfanyakazi,” aliongeza.



Rutasingwa alitoa wito kwa wafanyakazi wa benki hiyo kuendelea kuonyesha moyo wa ushirikiano na ubunifu, akisisitiza kuwa mafanikio haya ni matokeo ya juhudi za pamoja. “Benki ya CRDB si tu sehemu ya kazi – ni familia inayowekeza katika ndoto na ustawi wa kila mmoja wetu. Ushindi huu unathibitisha dhamira yetu ya kuweka viwango vipya vya ubora,” alisema.

Kupitia tuzo hizo za Top Employer, Rutasingwa amewahakikishia wadau, wateja, na washirika wa Benki hiyo kuwa itaendelea kuwekeza katika ubora wa wafanyakazi wake, lakini pia katika huduma na bidhaa ili kukuza ustawi wa watu wake na jamii kwa ujumla.


Friday, 17 January 2025

NMB BANK NAMED TOP EMPLOYER IN TANZANIA FOR THE YEAR 2025

NMB Bank's Chief Human Resources Officer, Emmanuel Akonaay (centre) displays the Tanzania Top Employer of the Year 2025 Award presented by Netherland's based Top Employers Institute. With him is the Bank's Head of Human Resourse Projects & Change Management - Ms. Juliana Muwanga (left) and Senior Relationship Manager, Agri Wholesale - Ms. Norma Shindika. 

COCA-COLA KWANZA SCOOPS TOP EMPLOYER AWARD FOR 2025

Coca Cola Beaverages Africa, Tanzania leaders pose with the Top Employer Award. From left to right - Emmanuel Kyarwenda, Fatma Mnaro Jonathan Jooste, Scolastika Augustine, Haji Ali, Hassan Waziri and Salum Nassor.

17 January 2025, Dar es Salaam; Coca-Cola Beverages Africa (CCBA) in Tanzania is one of only eight companies in Tanzania to be certified as a Top Employers for 2025 based on the results of the Top Employers Institute’s HR Best Practices Survey.

CCBA was certified as a Top Employer at the regional Africa level, and at the country level, for operations in Uganda, South Africa, Tanzania and Ethiopia.

“CCBA’s continued market success in Tanzania and our status as the largest bottler on the continent of beloved Coca-Cola brands, are other key differentiators,” said CCBA in Tanzania Acting General Manager, Jonathan Jooste.

“Our people are driven to make an impact, are passionate about learning and committed to caring for others
.

“We have a people-first culture that ensures exceptional professional development for our valued employees. Our aim is to nurture potential, attract and retain high-performing talent, and invest in growth.

“We empower individuals to thrive and our certification as a Top Employer reflects the strength of our commitment to being an employer of choice for professionals with a desire to learn and grow,” Jooste said.

“Congratulations to our leaders and colleagues and thank you for making this recognition possible.”

Thursday, 16 January 2025

NMB TAASISI YA KWANZA TANZANIA KUTAMBULIWA KAMA MWAJIRI KINARA 2025


Benki ya NMB imekuwa Taasisi ya Kwanza ya Kitanzania kupata ithibati ya kuwa Mwajiri Kinara Tanzania kwa Mwaka 2025, inayotolewa na taasisi bobevu na mahiri ya masuala ya rasilimali watu ya Top Employers Institute ya Uholanzi, ambayo kwa mwaka huu imetoa vyeti vya uKinara kwa taasisi bora katika nchi 124 duniani.


Hii sio mara ya kwanza NMB kutambulika kama Mwajiri Kinara, kwani tayari imetunukiwa Tuzo ya Mwajiri Bora Tanzania kwa Mwaka 2023 na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), lakini pia ilipata Tuzo ya Mwajiri Bora Afrika Mwaka 2022 kutoka Employer Branding Institute, taasisi bobevu ya masuala ya ajira duniani.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Alhamisi ya Januari 16, Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya NMB, Emmanuel Akonaay, alisema ni fahari kwa taasisi yake kuwa miongoni mwa mashirika 2,400 duniani yaliyotambuliwa na kutunukiwa uthibitisho huo wa uKinara kwa mwaka 2025.


Alibainisha kuwa, Top Employers Institute ni taasisi kinara duniani katika kufanya tafiti na ukaguzi huru wa mashirika kuhusu rasilimali watu, ikitumia vigezo vya kimataifa na wanajivunia tuzo hiyo ambayo inathibitisha kuwa NMB ni taasisi imara ya ajira na kiongozi katika maendeleo ya rasilimali watu nchini.


"Tuzo hii kutoka Top Employers Institute ni muhimu sana kwetu kama mwajiri wa takribani watu 4,000, kwani wafanyakazi walio tayari kujitolea na wenye motisha wa kuhudumia, ni msingi wa huduma Kinara na mojawapo ya njia kuu za kuwaridhisha wateja wetu".


“Uthibitisho wa Mwajiri Kinara unathibitisha thamani ya juhudi zetu na kuimarisha shauku yetu ya kuhakikisha kila mtu anafanikiwa".


“Pia, hii tuzo inayoakisi ahadi yetu ya mazingira Kinara kazini, yenye ustawi kwa wafanyakazi, ambao wanajivunia na kufurahia ajira zao. Kama sehemu ya mkakati wetu wa biashara, tunafanya uwekezaji mkubwa wa kuwa na utamaduni jumuishi ambapo watu wetu wanahisi kuthaminiwa na kushirikishwa," alibainisha Akonaay.


Aliongeza ya kwamba, kuna sababu kadhaa zilizowawezesha kutwaa tuzo hiyo, ikiwemo kuwa na mikakati bora juu ya wafanyakazi, upatikanaji wa wafanyakazi bora, uendelezaji wa wafanyakazi, namna bora ya kuwatumia wafanyakazi kulingana na ubora wao, utofauti na ujumuishaji na ustawi wa wafanyakazi.


Akonaay aliongeza kuwa kwa mwaka huu 2025, Taasisi ya Top Employers imetoa vyeti vya uKinara kwa taasisi mbalimbali katika nchi 124 duniani, ambazo kwa pamoja zina athari chanya kwenye maisha ya zaidi ya wafanyakazi zaidi milioni 13 kupitia mbinu Kinara za Rasilimali Watu na Mazingira Kinara ya Ajira.


“Kutunukiwa huku kwa Benki ya NMB kumetokana na kushiriki katika utafiti wa ‘Mbinu Kinara za Rasilimali Watu,’ ulioendeshwa na Top Employers Institute, kwa kuzingatia viwango vya kimataifa na kuwalinganisha washiriki kwa vigezo vya mbinu Kinara za ajira zinazotambulika na kutumika duniani".