Timu ya Vodacom Tanzania Plc Kanda ya Ziwa imeendelea kuonesha ukaribu na kuthamini wateja wake baada ya kujitokeza katika viwanja vya Soko la Samaki Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kugawa vikapu vya sikukuu kwa wateja na wakazi wa jiji hilo.
Katika tukio hilo, timu ya Vodacom ilikutana ana kwa ana na wateja wao, kuwashukuru kwa kuendelea kutumia huduma za kampuni hiyo pamoja na kuwapatia zawadi maalum za msimu wa sikukuu. Ugawaji huo umeonesha dhamira ya Vodacom kuendelea kujenga uhusiano mzuri na jamii, sambamba na kuongeza furaha katika msimu huu wa mwisho wa mwaka.
Mwanza ni miongoni mwa maeneo ambayo Vodacom imekuwa ikifanya matukio ya kujumuika na wateja, ikiwa ni sehemu ya kampeni za msimu wa sikukuu zinazolenga kutoa shukrani na kuongeza thamani kwa watumiaji wa huduma zake.
Kwa wakazi wa Kirumba na maeneo ya jirani, tukio hili lilikuwa fursa ya kipekee ya kukutana na timu ya Vodacom, kupata zawadi, pamoja na kufahamu zaidi huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
No comments:
Post a Comment