Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Friday, 10 October 2025

SERENGETI BREWERIES NA NCT ARUSHA WAZINDUA PROGRAMU YA “LEARNING FOR LIFE” KWA VIJANA

Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Kampasi ya Arusha kimefurika ari, tabasamu na matumaini mapya baada ya wanafunzi na wakufunzi kuanza rasmi safari yao kupitia programu ya Learning for Life, ushirikiano kati ya Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) na NCT unaolenga kuwawezesha vijana wa Kitanzania kupata ujuzi wa vitendo katika sekta ya ukarimu na utalii.

Zaidi ya vijana 160 wamejiunga na kundi hili jipya la mafunzo, wakiwa na hamasa kubwa ya kujifunza na kubadili ndoto zao kuwa uhalisia. Tangu siku ya kwanza, vyumba vya madarasa na maeneo ya mafunzo yamejaa nishati chanya, ushirikiano na hamu ya kujifunza.

Wanafunzi wanajifunza huduma kwa wateja, uandaaji wa vinywaji (mixology), na uongozi, yote yakiwa yamelenga kuwaandaa kwa ajira katika hoteli, migahawa na baa kwenye ukanda wa kaskazini wa utalii.

Kwa wanafunzi wengi, programu hii ni zaidi ya mafunzo — ni nafasi ya kujiamini, kukuza taaluma, na kufungua milango ya mafanikio katika maisha yao.

Wakufunzi nao hawakubaki nyuma katika furaha hii. Kupitia mfumo wa Training of Trainers (ToT) unaofadhiliwa na SBL, walimu wa NCT wamewezeshwa kutoa mafunzo ya kiwango cha juu yanayochanganya nadharia na vitendo, kuhakikisha kila mwanafunzi anaondoka akiwa tayari kwa soko la ajira.

Kadri mafunzo yanavyoendelea, jambo moja limekuwa wazi — ari, bidii na mshikamano vinavyoonekana NCT Arusha ni ishara ya mustakabali mzuri wa sekta ya ukarimu nchini Tanzania. Kupitia ushirikiano huu, SBL na NCT hawatoi tu mafunzo, bali wanaunda kizazi kipya cha vijana wenye uwezo wa kuhudumia, kuongoza na kuhamasisha wengine.



No comments:

Post a Comment