Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Wednesday, 8 October 2025

DCB YAZINDUA KAMPENI YA “TUKO GROUND NA WENYEWE” KUONGEZA UJUMUISHAJI WA KIFEDHA

Dar es Salaam, 7 Oktoba 2025 – Benki ya DCB Commercial Bank Plc imezindua rasmi kampeni yake mpya iitwayo “Tuko Ground na Wenyewe”, yenye lengo la kuongeza ujumuishaji wa kifedha na kuhamasisha matumizi ya huduma za kidigitali nchini Tanzania.

Kupitia kampeni hiyo, wateja wataweza kufungua akaunti kwa njia ya mtandao popote walipo na kutuma fedha bure kwenda benki nyingine au mitandao ya simu — hatua inayolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa Watanzania wa kipato cha chini na cha kati.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Sabasaba Moshingi, Mkurugenzi wa Mikopo na Hatari za Kibenki, Deogratius Tadei, alisema kampeni hiyo inalenga kupunguza gharama za huduma za kifedha na kuwawezesha wananchi wengi zaidi kujiunga na mfumo rasmi wa kibenki.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Huduma kwa Wateja na Huduma za Kidigitali wa DCB, Geophrey Magugi, alisema kampeni hiyo inaendana na mkakati wa serikali wa kujenga uchumi wa kidigitali kwa kuhamasisha jamii kutumia mifumo ya malipo isiyotumia fedha taslimu. Aliongeza kuwa huduma hizo zitachochea matumizi ya teknolojia katika miamala ya kifedha na kuongeza ufanisi katika sekta hiyo.

Johanes Msuya, Katibu wa Mradi kutoka Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), aliipongeza DCB kwa ubunifu huo, akisema utachangia kuongeza ushiriki wa wananchi katika huduma za kifedha rasmi.

Kwa upande wake, mteja wa DCB, Salma Athman, alisema huduma hizo mpya zitasaidia kupunguza muda na gharama za kupata huduma za kifedha, hasa kwa wananchi wanaoishi maeneo ya pembezoni.

Kampeni ya “Tuko Ground na Wenyewe” inaonyesha dhamira ya DCB katika kukuza ujumuishaji wa kifedha, ubunifu, na kuwawezesha wateja kupitia huduma bora za kidigitali.





No comments:

Post a Comment