Suluhisho Maalumu kwa Wahandisi, Mafundi na Wafanyakazi wa Migodi
Geita, Tanzania – Ijumaa, 12 Septemba 2025:
Geita ni kiini cha sekta ya madini nchini Tanzania, ikiwa makazi ya maelfu ya wanaume na wanawake wanaochangia ukuaji wa uchumi wa taifa. Kwa kutambua mchango wao, Benki ya Stanbic Tanzania imetangaza kujidhatiti katika kuwawezesha wafanyakazi wa migodini Geita kupitia suluhisho bora za kifedha zinazowawezesha kustawi, kuwekeza na kujenga mustakabali wa kudumu.
Mikopo ya Nyumba, Magari na Vifaa
Katika hafla maalumu ya wafanyakazi wa migodini, Stanbic ilitambulisha rasmi huduma za kifedha zikiwemo:
- Mikopo ya nyumba yenye thamani hadi TZS bilioni 1.2, muda wa marejesho hadi miaka 20.
- Straight purchase loans ambapo benki inafadhili hadi 90% ya thamani ya nyumba.
- Takeover mortgages kwa masharti nafuu zaidi.
- Mikopo ya magari na vifaa – kuanzia magari binafsi, mabasi, hadi vifaa vya migodini kama excavators, bulldozers na drilling rigs.
“Geita siyo tu kitovu cha madini, ni jamii ya watu wenye maono makubwa wanaoendesha gurudumu la uchumi wa Tanzania,” alisema Emmanuel Mahodanga, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Stanbic Tanzania.
Akiba, Uwekezaji na Bima
Zaidi ya mikopo, Stanbic pia imetambulisha:
- Mikopo ya ujenzi wa nyumba
- Huduma za akiba na uwekezaji
- Bima ya mikopo (credit life insurance) kuhakikisha wafanyakazi wanajenga mali huku wakilinda familia zao.
Sehemu ya Safari ya Miaka 30 ya Stanbic Tanzania
Hatua hii ni mwendelezo wa safari ya miaka 30 ya Benki ya Stanbic nchini Tanzania chini ya kaulimbiu “Tanzania Mabegani – Miaka 30 ya Kukua Pamoja.” Benki inaendelea kuthibitisha nafasi yake kama mshirika wa ustawi wa kifamilia, maendeleo ya jamii na mageuzi ya kiuchumi nchini.
“Wafanyakazi wa migodini Geita ni nguzo ya ukuaji huo, na tunajivunia kutembea nao katika safari hii, tukiwawezesha kufanikisha malengo yao,” alihitimisha Mahodanga.
.jpeg)

No comments:
Post a Comment