Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Saturday, 16 August 2025

TBL YAWEZESHA WAKULIMA WA SHAYIRI MONDULI JUU KUONGEZA UZALISHAJI NA UBORA

Monduli Juu, Arusha – 15 Agosti 2025: Tanzania Breweries Plc (TBL) imefanya mafunzo ya vitendo kwa wakulima wa shayiri Monduli Juu, Arusha, ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuendeleza kilimo cha shayiri nchini. Zaidi ya wakulima 200 walihudhuria katika Siku ya Wakulima wa Shayiri, tukio lililoambatana na Shamba Darasa na majadiliano ya changamoto za kilimo.

Hafla hiyo iliudhuriwa na viongozi wa serikali akiwemo Katibu Tawala wa Wilaya ya Monduli, Mheshimiwa Muhsin Kassim, ambaye alisisitiza dhamira ya serikali kuimarisha upatikanaji wa pembejeo bora, huduma za ugani na masoko yenye tija.

“Wakulima ndiyo uti wa mgongo wa taifa letu. Leo tunathibitisha dhamira yetu ya kuwasaidia kupitia utafiti, huduma bora na masoko salama,” alisema Mheshimiwa Kassim.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria na Mahusiano wa TBL, Bi. Neema Temba, alisema kampuni itaendelea kuunga mkono wakulima wadogo kwa mikataba ya mauzo na mafunzo ya kitaalamu.

“Matukio kama haya yanatukumbusha nafasi muhimu ya wakulima siyo tu katika usalama wa chakula, bali pia katika kuendeleza viwanda kama chetu,” alisema Bi. Temba.

TBL ni mnunuzi mkubwa wa shayiri nchini na imekuwa ikishirikiana na wakulima wadogo kwa muda mrefu ili kuongeza tija na kuhakikisha malighafi za ndani zinatumika katika viwanda vyake vya bia.

Miongoni mwa mada zilizojadiliwa ni pamoja na mabadiliko ya tabianchi, upotevu wa mazao baada ya mavuno na upatikanaji wa pembejeo bora. Wadau walikubaliana kuimarisha ushirikiano kati ya sekta binafsi, serikali na wakulima kwa ajili ya kilimo endelevu cha shayiri na masoko thabiti.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na:

Neema Temba
Mkurugenzi wa Masuala ya Uhusiano wa Kampuni – TBL
📧 tblcorporate.communications@ab-inbev.com







No comments:

Post a Comment