Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Wednesday, 27 August 2025

PUMA ENERGY YAWASHAURI TAASISI ZA UMMA KUBORESHA UTENDAJI NA HUDUMA

Dar es Salaam – Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Bi. Fatma M. Abdallah, ametoa rai kwa Taasisi za Umma (SOEs) kuachana na urasimu na kuzingatia mbinu bunifu za kisasa zitakazoharakisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Akizungumza mbele ya Wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi Wakuu wa mashirika ya umma, Bi. Abdallah alisisitiza umuhimu wa kuanzisha mifumo thabiti inayojengwa juu ya utawala bora, uwazi, matumizi sahihi ya data, biashara endelevu na viashiria vya utendaji (KPIs) ili kuongeza ufanisi na matokeo bora ya huduma.

Kwa upande wa Puma Energy Tanzania, Bi. Abdallah alisema kampuni inajivunia mafanikio chanya yaliyopatikana kupitia mfumo wa nguzo tano unaojikita katika:

  1. Uongozi thabiti
  2. Mageuzi ya sera
  3. Miundombinu ya kidijitali
  4. Nguvu kazi yenye wepesi
  5. Utamaduni wa utendaji unaoendeshwa na matokeo

Kupitia mfumo huu, Puma Energy imeweza kuboresha huduma zake, kuongeza ufanisi na kuendelea kujenga imani kwa wadau wake.

No comments:

Post a Comment