Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 1 November 2024

UBORESHAJI WA MAMLAKA YA BANDARI KUONGEZA IDADI YA ABIRIA ZIWA VICTORIA


Mwanza: Idadi ya abiria wanaosafiri katika Ziwa Victoria inatarajiwa kuongezeka mara mbili mwaka ujao, kutokana na miradi mikubwa ya upanuzi wa bandari na uzinduzi unaosubiriwa wa meli ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu, meli yenye uwezo mkubwa wa kubeba abiria na mizigo.


Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Bw. Erasto Lugenge, alisema Alhamisi kuwa maboresho haya, yanayoungwa mkono na uwekezaji wa serikali ya Tanzania wa Sh60 bilioni, yanatarajiwa kubadilisha usafiri katika Kanda ya Ziwa.


Kwa sasa, bandari za Ziwa Victoria zinahudumia takribani abiria milioni 1.64 kila mwaka. Hata hivyo, kwa miundombinu mipya, idadi hii inatarajiwa kuongezeka mara mbili. Akizungumza na waandishi wa habari katika Bandari ya Mwanza Kaskazini, Bw. Lugenge alifafanua mgawanyo wa uwekezaji wa serikali: Sh18.6 bilioni zimetengwa kwa Bandari ya Mwanza Kaskazini, huku fedha zilizobaki zikienda kwenye bandari za Kemondo na Bukoba.


Maboresho hayo yameundwa ili kuweza kumudu MV Mwanza Hapa Kazi Tu, ambayo itakuwa meli kubwa zaidi ya abiria Afrika Mashariki baada ya kukamilika. Meli hii yenye urefu wa mita 92, bado inajengwa, na inatarajiwa kubeba abiria 1,200, tani 400 za mizigo, magari madogo 20, na malori makubwa matatu. Hii ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na meli ya sasa ya MV Victoria yenye uwezo wa kubeba abiria 600.


Mapato kutoka bandari za Kanda ya Ziwa pia yanatarajiwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa. Kwa sasa, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) inakusanya Sh4 bilioni kutoka shughuli za Kanda ya Ziwa, ambapo baada ya maboresho haya, kiasi hiki kinatarajiwa kuongezeka hadi Sh8 bilioni.


Mradi wa kuboresha bandari ulianza Mei mwaka jana na ulipangwa kukamilika ndani ya miezi 18, ingawa kwa sasa uko asilimia 44 ya utekelezaji. Bw. Lugenge alieleza kuwa kulikuwa na kuchelewa kidogo, kwani baadhi ya mabadiliko yalihitajika ili kukidhi mahitaji ya usanifu wa MV Mwanza Hapa Kazi Tu.

ECOBANK AIDS WOMEN CONTRACTORS ASSOCIATION CONFERENCE 2024

The Chief Guest, Amb. Eng. Aisha Amour, Permanent Secretary, Ministry of Works (second right) presents an appreciation award to Joyce Ndyetabura, Head of Commercia Banking, Ecobank Tanzania.

Ecobank Tanzania, Dar es Salaam, 31st October 2024 – Ecobank Tanzania, an affiliate of Ecobank Group, the leading pan-African banking group, supported the Women contactors Conference which took place on 31st October, 20024 at Julius Nyerere International Convention Center (JNICC) in Dar es Salaam. 
 
Joyce Ndyetabura, Head of Commercial Banking at Ecobank Tanzania, speaks at the event.
The Tanzania Women Contractors Association (TWCA) is a voluntary nonprofit organization established under the Societies Act CAP.337 R.E.2002 with the Ministry of Home Affairs. Their mission is to advocate for women's active involvement in the construction and affiliated sectors, challenge stereotypes, and foster a more inclusive environment. They collaborate closely with government bodies, regulatory boards, international organizations, national universities, and the private sector.



Tanzania Women Contractors Association (TWCA) conducts its annual Conference and General Meeting each year, this year’s event, themed "Empowering Women Contractors: Building Local Strength, Creating Global Impact," The event brought together around 300 participants.


This year's conference aims to empower women contractors through capacity building, promote local content and sustainability, foster networking and collaboration opportunities and advocate for supportive policies and fair contract terms. The chief guest was Amb. Eng. Aisha Amour Permanent Secretary, Ministry of Works, who represented the Minister for Works, Hon. Innocent Bashungwa.


This is a great platform for the bank to in line with our Trade Strategy, promoting guaranteed business and Elevate program aiming at increasing our balance sheet through our working capital solutions.

UJUMUISHWAJI NA USHIRIKISHWAJI WA WANAWAKE, WENYE ULEMAVU WASISITIZWA KUONGEZA KASI YA MAENDELEO

Shabnam Mallick, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa akikata utepe kufungua kapu lililobeba ripoti ya uendelevu ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) kwenye shughuli iliyofanyika jijini Dar es Salaam siku ya Alhamisi, 31 Oktoba. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Obinna Anyalebechi na wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya SBL, Paul Makanza.

Dar es Salaam, Oktoba 31, 2024. Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL) imezindua rasmi Ripoti yake ya Uendelevu ya 2024 yenye kaulimbiu ‘Kusimamia Ujumuishwaji na Ushirikishwaji’, mnamo Oktoba 31, 2024. Ripoti hii inaangazia dhamira ya SBL ya kuendeleza mazingira jumuishi ambapo watu wenye asili mbalimbali wanaweza kufanikiwa, kwa kuzingatia kuondoa vikwazo na kuleta athari chanya kwa jamii, wasambazaji, na wadau.


SBL, ikifanya kazi chini ya East African Breweries Limited (EABL), imepanga kutenga rasilimali za kutosha kuwekeza katika jamii kupitia mpango wao wa ‘Spirit of Progress’ - mpango wa ESG unaolenga kuunda jamii endelevu katika maeneo wanayoyahudumia. Tukio hilo liliwakutanisha mamia ya wadau na kufanya mazungumzo kuhusu namna ya kuboresha ushirikiano ili kuendeleza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa kiuchumi kwa kushughulikia changamoto, fursa, na uboreshaji wa sera.


Shabnam Mallick, Mkuu wa Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), alihudhuria tukio hilo na kutoa mtazamo wake, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano, uboreshaji wa sera, na hatua za pamoja katika kuendeleza usawa wa kijinsia kama nguzo ya uwezeshaji kiuchumi na uendelevu katika taasisi yoyote.


"Ninafurahi kuona hatua kubwa ambazo SBL imepiga katika kukuza usawa wa kijinsia na kuunga mkono wanawake katika nafasi za uongozi. Ninafurahia pia kuona kwamba kampuni imeweka malengo ya matumizi kwa wasambazaji mbalimbali pamoja na ufuatiliaji. Hiki ni kitendo cha makusudi ambacho ni muhimu katika kufikia malengo yetu ya muda mrefu ya uendelevu na kuhakikisha maendeleo yanawafikia wote," alisema Mallick.


Mwenyekiti wa Bodi ya SBL, Paul Makanza alikazia mbinu zinazotumika kuhakikisha ripoti za uendelevu zinakuwa chachu ya maendeleo kiuchumi Afrika, alisema, ‘Wanawake wanapokuwa na fursa sawa, uchumi unakua, familia zinastawi, na jamii zinaendelea. Tukifunga pengo la kijinsia barani Afrika, inaweza kuongeza dola bilioni 316 kwenye uchumi wetu kufikia mwaka 2025. Huo ndio ukuaji. Na hii ni sehemu ambayo SBL tumedhamiria kuhusika zaidi’.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Obinna Anyalebechi, alizungumzia mchango wa kampuni yao kwenye ukuaji jumuishi na uwezeshaji kiuchumi wa makundi maalum nchini, akisema, “Juhudi zetu za ushirikishwaji na usawa zinaakisi dhamira yetu ya kuwezesha makundi yaliyotengwa, ikiwa ni pamoja na wanawake, watoto, na watu wenye ulemavu, ili wafaidike na fursa za kijamii na kiuchumi. Najivunia kuripoti kwamba karibu asilimia 40 ya wakulima tuliowawezesha mwaka huu walikuwa ni wanawake na watu wenye ulemavu ambao wanalima mtama, moja ya viungo muhimu katika uzalishaji wa bia zetu. Kupitia ushirikiano wetu na Sightsavers, tumewaunga mkono zaidi ya wanawake na watu wenye ulemavu 200 katika mkoa wa Singida, tukiwasaidia kukuza mtama kwa ajili ya uzalishaji kwa SBL.”


Ripoti hii inaeleza zaidi mipango ya kimkakati ya SBL inayolenga kuondoa vikwazo vinavyozuia ushirikishwaji na maendeleo, hasa kwa wanawake na watu wenye ulemavu. Mipango hii, ambayo inaambatana na ahadi kubwa za ESG za SBL, inachangia kwa kiasi kikubwa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs).

VODACOM TANZANIA YAFANYA MABORESHO MAKUBWA YA MTANDAO WAKE


Dar es Salaam – 29 Oktoba 2024: Kampuni kinara ya teknolojia na mawasiliano nchini, Vodacom Tanzania, imetangaza kufanya mabadiliko makubwa katika miundombinu ya mtandao wake ikiwa ni sehemu ya kuwahakikishia wateja wake huduma bora na za kisasa zaidi.

Akizungumzia hatua hii, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Philip Besiimire alisema kuwa Vodacom imejidhatiti kuwa kinara katika ubunifu na kuboresha huduma zake kila wakati. “Ili kuendelea kuwa kinara katika teknolojia na kuwapatia wateja wetu huduma bora, tumewekeza kwa kiwango kikubwa katika kuboresha miundombinu ya mtandao wetu,” alibainisha.

Hatua hii ni muhimu kwa kuwa inaiandaa nchi na wateja wetu kuwa tayari kupokea mabadiliko ya teknolojia ya kisasa kama vile Akili Mnemba (AI) ambayo inalenga kuleta maboresho makubwa ya upatikanaji wa huduma za mtandao kwa wateja.

Besiimire alifafanua kuwa maboresho haya yanalenga kuongeza kasi, kuimarisha mtandao na kuhakikisha huduma zinaendelea kubaki imara ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka kila kukicha. Ingawa jitihada hizi ni hatua kubwa mbele, pia zinapitia mchakato mgumu ambao unaweza kuathiri upatikanaji wa huduma katika maeneo kadhaa kwa kiasi fulani.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote ambao umewaathiri wateja wetu na tunawahakikishia kwamba tunafanya kila jitihada kupunguza usumbufu huo. Zoezi hili linatarajiwa kukamilika ifikapo katikati ya Novemba, ambapo tutakuwa na mtandao wenye nguvu na unaotegemewa zaidi kwa manufaa ya wateja wetu wote,” alisema huku akiongeza kuwa timu yake itaendelea kuufahamisha umma wakati wote wa zoezi hili na kutoa msaada wowote utakapohitajika.

VODACOM YAUNGANA NA BOLT KUKUZA UJUMUISHWAJI WA KIFEDHA KIDIJITALI

Mkuu wa Idara ya Lipa kwa Simu wa Vodacom Tanzania Plc, Kilian Kamota (kushoto), Mkurugenzi wa M-Pesa Epimack Mbeteni (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Bolt Tanzania Dimmy Kanyankole (wa pili kulia) na Meneja Mwandamizi wa Bolt Milu Kipimo wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya Vodacom na kampuni ya Bolt wenye lengo la kuongeza ujumuishwaji wa kifedha nchini katika tukio lililofanyika tarehe 29 Oktoba jijini Dar es Salaam.
  • Kutoa mikopo ya simu, bima za aina mbalimbali na mafuta kwa madereva, ili kuwawezesha kutoa huduma bora zaidi
Dar es Salaam – 29/10/2024: Vodacom Tanzania Plc imetangaza ushirikiano wa kimkakati na Bolt, moja kati ya makampuni makubwa ya teksi mtandao, wakitoa huduma za usafiri nchini, kwa lengo la kuongeza ujumuishwaji wa kifedha kwa madereva na kukuza malipo ya kidijitali. Ushirikiano huu utaleta huduma za miamala ya kifedha kidijitali kwa madereva wa Bolt, wakiwemo madereva wa Magari, Bajaj na Bodaboda, kupitia mfumo wa M-Pesa kutoka Vodacom.


Ushirikiano huu utatoa fursa za kipekee kama mfumo wa malipo bila kutumia fedha taslimu wa ‘Lipa kwa Simu’, mikopo ya simu, aina mbalimbali za bima, mikopo ya wafanyabiashara na mkopo wa mafuta wa Chomoka, iliyotengenezwa mahsusi ili kuwawezesha madereva wa Bolt kutumia fedha zao kiusalama na kwa faida. Huduma hizi zitawarahisishia madereva utaratibu wa malipo na pia kuwasaidia kupata huduma muhimu kama vile matengenezo ya magari, mafuta na bima za vyombo vya moto.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa M-Pesa Vodacom Tanzania, Epimack Mbeteni, alisema, “Ushirikiano huu unaleta mabadiliko makubwa kwa madereva na wateja pia. Kupitia Lipa kwa Simu, tunawawezesha madereva wa Bolt kutumia mfumo salama, rahisi, na usio wa malipo ya fedha taslimu ambao utawawezesha kuongeza kipato chao na kupata huduma muhimu kama mikopo ya mafuta na bima za aina mbalimbali. Hatua hii ni sehemu ya jitihada zetu za kujenga mfumo thabiti wa malipo bila fedha taslimu na kukuza ujumuishwaji wa kifedha hapa nchini.”


Naye Meneja Mkuu wa Bolt, Dimmy Kanyankole, alibainisha faida za ushirikiano huu kwa madereva na wateja wa Bolt, "tunafurahi kushirikiana na Vodacom Tanzania Plc kwa kuunganisha huduma za M-Pesa na huduma za usafiri wa Bolt. Ushirikiano huu utafanikisha mchakato wa malipo kuwa rahisi zaidi kwa madereva wetu na wateja, huku pia tukitoa huduma za ziada za kifedha zinazosaidia kuinua Uchumi wa madereva. Tunaamini ushirikiano huu utaimarisha sana ustawi wa madereva wetu na kuboresha huduma kwa watumiaji wa Bolt nchini Tanzania."


Kupitia ushirikiano huu, Vodacom Tanzania na Bolt wanakusudia kuongeza thamani na idadi ya miamala ya kidijitali huku wakipanua wigo wa huduma za kifedha kwa madereva wa Bolt na jamii kwa ujumla. Kwa kutoa mikopo, bima na kurahisisha huduma za malipo, ushirikiano huu unaunga mkono uwezeshaji wa kidijitali na kiuchumi kwa Watanzania.