Arusha, Agosti 25, 2025 – Benki ya NMB imedhamini na kushiriki kwenye Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma (CEOs Forum 2025) kinachoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC).
Ujumbe wa NMB katika kikao hicho unaongozwa na David Nchimbi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, pamoja na Juma Kimori, Afisa Mkuu wa Fedha na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu.
Kikao kazi hicho cha siku tatu kimewakutanisha viongozi zaidi ya 650 kutoka Taasisi, Mashirika na Wakala wa Serikali, kwa lengo la kujadili masuala muhimu ya kiutendaji na kimkakati yanayohusu taasisi za umma nchini.
Kaulimbiu ya kikao hicho ni:
“Kujenga Ushirikiano Endelevu katika Mazingira ya Ushindani wa Kimataifa – Wajibu wa Mashirika ya Umma.”



.jpeg)
.jpeg)
No comments:
Post a Comment