Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

Friday, 16 May 2025

NBC YAWAFIKIA WAKULIMA WA UFUTA LINDI NA MTWARA KUPITIA KAMPENI YA “NBC SHAMBANI”

Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bi Victoria Mwanziva (alieshika mkasi) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima zao la ufuta mkoani Lindi na wilaya za Masasi na Nanyumbu mkoani Mtwara wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika mapema jana mkoani Lindi. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Biashara wa benki ya NBC Bw Joseph Lyuba (watatu kulia) Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa (kulia), Meneja wa NBC tawi la Lindi Bw Iovin Mapunda (wa pili kulia), Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Lindi Bw Keneth Shemdoe (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Lindi Mwambao Bw Hassan Mnumbe (kushoto).
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bi Victoria Mwanziva (kulia) akipokea zawadi maalum ya fulana na kofia zenye kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Biashara wa benki ya NBC Bw Joseph Lyuba (wa pili kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima zao la ufuta mkoani Lindi na wilaya za Masasi na Nanyumbu mkoani Mtwara iliyofanyika mapema jana mkoani Lindi.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bi Victoria Mwanziva (kulia) akizungumza na wadau wa kilimo wakiwemo wakulima kutoka mkoa wa Lindi wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ inayoratibiwa na benki ya NBC.
  • Yasisitiza dhamira yake kukuza uzalishaji mazao ya kilimo
Lindi, Mei 16, 2025: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), imetambulisha kampeni yake ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ kwa wakulima wa zao la ufuta mkoa wa Lindi na Wilaya za Masasi na Nanyumbu mkoani Mtwara huku ikikisistiza dhamira yake ya kuunga mkono azma ya serikali ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo kutoka asilimia 5 hadi 10 ifikapo mwaka 2030.


Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo imefanyika leo mkoani Lindi ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bi Victoria Mwanziva. Pia walikuwepo wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara akiwemo Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Lindi Bw Keneth Shemdoe, viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika vya wakulima na wafugaji (AMCOS), pamoja na wadau wengine wanaoshiriki kwenye mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo.


Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Biashara wa benki ya NBC Bw Joseph Lyuba na Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa waliwaongoza maofisa wengine wa benki hiyo kwenye uzinduzi wa kampeni ambayo ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuchochea kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo kupitia uchumi jumuishi unaochagizwa na huduma rasmi za kifedha.


Akizungumza kwenye hafla hiyo, Bi Mwanziva aliitambua benki ya NBC kama mdau muhimu kwenye maendeleo ya sekta ya kilimo nchini hususani mikoa ya kusini ambapo benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kuendesha kampeni za namna hiyo zenye lengo la kuchochea kasi ya uzalishaji wa mazao ya korosho na ufuta sambamba na kuwajengea uelewa wananchi kuhusu elimu ya fedha.


Nimefarijika sana kuona kwamba kupitia kampeni hii NBC zaidi ya milioni 30 zimetengwa kwa ajili ya zawadi mbalimbali mahususi kwa wakulima ikiwemo vitendea kazi vya shughuli za kilimo. Hamasa hii ni msaada mkubwa kwa serikali kwa kuwa kilimo kinaongeza ajira na zaidi elimu wanayoipata wakulima kupitia kampeni ni msaada zaidi katika kufanikisha azma ya kilimo cha kisasa sambamba na kuongeza uelewa wa masuala ya fedha kwa wananchi…tunawashukuru sana NBC,’’ alisema.


Akizungumza kwenye uzinduzi huo Bw Lyuba alisema ili kufanikisha dhamira yake ya kuunga mkono azma ya serikali ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo kutoka asilimia 5 hadi 10 ifikapo mwaka 2030, benki hiyo inaendelea kubuni na kuboresha huduma mbalimbali za kifedha kwa ajili ya wadau mbalimbali wa sekta kilimo nchini wakiwemo wakulima.


PUMA ENERGY, AMEND WASHIRIKIANA KUELIMISHA WANAFUNZI KUPITIA MAHAKAMA KIFANI YA WATOTO

Mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Kibugumo ya Kigamboni, Munir Said Mussa (12), katikati, akimhoji mmojawapo wa dereva aliyekamatwa nje ya barabara karibu na shule hiyo katika ‘Mahakama Kifani ya Watoto’ kwa kukiuka alama za barabarani ikiwa ni sehemu ya kampeni ya ‘Be Road Safe Africa’ inayoendeshwa na kampuni ya Puma Energy Tanzania na shirika la Amend nchini.

Katika kuadhimisha Wiki ya Usalama Barabarani Duniani (May 12 - 18, 2025), kampuni ya Puma Energy Tanzania kwa kushirikiana na shirika la Amend Tanzania wameendesha 'Mahakama Kifani ya Watoto' kuhusu usalama barabarani tukio ambalo ni sehemu muhimu ya programu ya kampeni ya elimu ya usalama barabarani kwa shule za msingi ambayo pia inajulikana kama ‘Be Road Safe Africa’. Tukio hilo lilifanyika katika Shule ya Msingi ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, kuanzia mwanzoni mwa wiki na kuhitimisha siku ya Ijumaa ya Mei 16.


Awamu ya kwanza ya kampeni ya ‘Be Road Safe Africa’, ilitekelezwa mwaka 2023 na 2024, ambapo iliwafikia watoto zaidi ya 38,000 katika shule 20 za nchini Tanzania, Botswana, Zambia, na Zimbabwe. Awamu ya pili itatekelezwa katika nchi za Tanzania, Botswana, Zambia, Zimbabwe, na Afrika ya Kusini. Kwa nchini Tanzania awamu hii imezinufaisha shule tano ambazo ni: Kisukuru (Tabata), Kunguru (Goba), Mjimpya (Kurasini), Ufukoni (Kigamboni), na Salasala (Salasala).


Kampeni ya mwaka huu imewafikia zaidi ya wanafunzi 6,960 kupitia njia rahisi na shirikishi za kujifunzia, ikiwemo simulizi za hadithi, michezo - inayohusiana na masuala ya usalama barabarani na ‘Mahakama ya Watoto’. Wakati wa mahakama hii, wanafunzi hujifanya kama ‘majaji wa usalama barabarani’ ili kuwasaidia madereva kuelewa umuhimu wa kuzingatia usalama. Cha kuvutia zaidi, zaidi ya wanafunzi 290 wa chekechea pia walikuwa miongoni mwa wanufaika wa elimu ya usalama barabarani kupitia mpango huo.


Katika vifo 31 kwa kila watu 100,000, WHO inaripoti kwamba vifo vinavyotokana na ajali za barabarani nchini Tanzania ni karibu mara 1.7 ya kiwango cha kimataifa na juu zaidi ya wastani wa Afrika. Takwimu za Jeshi la Polisi Tanzania zinaonyesha kuwa mwaka 2024 pekee, nchi ilirekodi ajali 1,735 za barabarani ambapo ajali 1,198 kati ya hizo zilisababisha vifo vya Watu 1,715. Makosa ya kibinadamu, ikiwemo kupuuzia alama za barabarani, kuendesha gari kwa uzembe, na mwendokasi, vilichangia 97% ya matukio haya.



Programu ya ‘Be Road Safe Africa’ ni sehemu ya dhamira ya Puma Energy Tanzania ya kusaidia usalama na ustawi wa jamii, hasa jamii zilizo katika mazingira magumu na maeneo hatarishi. Kupitia mafunzo ya mbinu mbalimbali, mashindano, na uboreshaji wa miundombinu, programu hii inasaidia kuzifanya barabara zetu kuwa salama kwa watoto wa shule nchini.

NBC YAKABIDHI KOMBE LA UBINGWA WA "NBC CHAMPIONSHIP" KWA MTIBWA SUGAR FC

Wachezaji wa timu ya Mtibwa Sugar FC, viongozi na wadau mbalimbali wakijipongeza baada ya timu hiyo kukabidhiwa rasmi kombe la Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) msimu wa 2024/2025. Hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa huo ilifanyika jana katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam ikipambwa na mechi ya kirafiki kati ya bingwa huyo na timu ya Mbeya City FC mechi iliyoisha kwa timu hizo kutoka suluhu ya 2-2.
Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo na Wakubwa wa benki ya NBC Elibariki Masuke (katikati) akikabidhi kombe la Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) kwa Makamu wa pili wa Rais wa TFF na Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) Steven Mguto (kushoto) ili aweze kulikabidhi kwa nahodha wa timu ya Mtibwa Sugar FC, Oscar Masai (kulia) baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa ligi ya NBC Championship msimu 2024/2025.
Makamu wa pili wa Rais wa TFF na Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) Steven Mguto (kushoto) akikabidhi kombe la Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) kwa nahodha wa timu ya Mtibwa Sugar Oscar Masai baada ya timu hiyo kuwa bingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa 2024/2025.
Makamu wa pili wa Rais wa TFF na Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) Steven Mguto (alievaa kanzu) akiongoza zoezi la uvalishaji wa medali kwa wachezai wa Mtibwa Sugar FC walioibuka mabingwa wa kombe la Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) msimu wa 2024/2025.
Mkurugenzi wa Idara ya Wateja Wadogo na Wakubwa wa benki ya NBC Elibariki Masuke (katikati) akiwapongeza wachezaji wa timu ya Mbeya City wakati wa hafla hiyo.

Dar es Salaam, Mei 16, 2025: Mdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekabidhi kombe la ubingwa wa ligi hiyo kwa timu ya Mtibwa Sugar FC yenye maskani yake Turiani, Mkoani Morogoro ambayo ndiyo bingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa 2024/2025.


Hatua hiyo inatoa ruhusa kwa mabingwa hao kushiriki Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League) katika msimu ujao wa 2025/2026 sambamba na timu Mbeya City FC kutoka jijini Mbeya ambayo imemaliza ligi hiyo ikiwa nafasi ya pili.


Hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa huo ilifanyika jana katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam ikipambwa na mechi ya hisani kati ya bingwa huyo na timu ya Mbeya City FC, mechi iliyoisha kwa timu hizo kutoka suluhu ya 2-2.


Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo na Wakubwa wa benki ya NBC Elibariki Masuke alimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi kwenye tukio hilo lililopambwa na uwepo wa wadau mbalimbali wa mchezo huo wakiwemo viongozi wa kisiasa na serikali pamoja na viongozi mchezo huo wakiongozwa na Makamu wa pili wa Rais wa TFF na Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) Steven Mguto.


ECOBANK TANZANIA BACKS CRB 2025 ANNUAL CONSULTATIVE MEETING

Joyce Ndyetabura (left), Ecobank Tanzania Head of Commercial Banking, receives a certificate of appreciation from Minister of Works, Hon. Abdallah Hamis Ulega (MP).

Ecobank Tanzania, Dar es Salaam, 15th May 2025: Ecobank Tanzania, an affiliate of Ecobank Group, the leading pan-African banking Group, was proud to support the 2025 CRB annual consultative meeting which took place on 15th and 16th May 2025 at Diamond Jubilee Hall, Dar es Salaam. The chief guest was Minister of Works Hon. Abdallah Hamis Ulega (MP).


The Contractors Registration Board (CRB) was established by the Contractors Registration Act CAP R.E 2002 with a mission to regulate and develop a competitive and sustainable construction industry with capable contractors who deliver quality works and observe safety in pursuit of economic growth.


Ecobank participated in this important event as part of its commitment to support the growth and transformation of the construction and infrastructure sector in the country. As a pan-African bank with presence in over 33 countries, Ecobank brings a wealth of experience in supporting large scale infrastructure projects and SMEs through innovative digital banking products, trade finance solutions and capacity building initiatives.


We recognize the vital role contractors play in driving national development and this is a great opportunity for the Bank to be able to reach out to many contractors and offer the right solutions for their businesses. We are committed to working hand in hand with industry players by offering tailored financial solutions that address the unique needs of contractors”, said Joyce Ndyetabura, Head of Commercial Banking.

More than 1,200 participants attended the meeting.




SBL KWA KUSHIRIKIANA NA NCT WAADHIMISHA MAHAFALI YA KWANZA YA UKARIMU KWA VIJANA


Dar es Salaam, Mei 16, 2025: Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL), kwa kushirikiana na Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), wamefanya mahafali ya kwanza ya programu ya mafunzo ya ukarimu kwa vijana chini ya mpango wa SBL wa "Learning for Life", wenye lengo la kuwajengea vijana wa Kitanzania ujuzi wa vitendo katika sekta ya ukarimu na utalii.


Mahafali haya, yaliyofanyika katika kampasi ya NCT jijini Dar es Salaam, yalikutanisha wanafunzi 109 waliohitimu, wadau wa sekta ya ukarimu, pamoja na viongozi wa serikali. Mgeni rasmi wa hafla hiyo alikuwa Mhe. Edward Mpogolo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, huku Mgeni Maalum akiwa ni Mhe. Dkt. Pindi Hazara Chana (Mb), Waziri wa Maliasili na Utalii.


Mpango huu ulioanza Septemba mwaka jana ni sehemu ya mkakati mpana wa SBL wa Society 2030: Spirit of Progress, ukilenga kuwawezesha vijana kupitia mafunzo ya vitendo, masomo darasani na mafunzo kwa vitendo kazini ili wawe tayari kuajiriwa kwenye soko la ajira linalokua la utalii na ukarimu.


Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Dkt. Pindi Chana alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya taifa kupitia utalii shirikishi:


Utalii siyo tu kusafiri – ni injini ya ukuaji wa uchumi jumuishi, ajira kwa vijana na kubadilishana tamaduni. Tanzania inalenga kufikia watalii milioni 5 kwa mwaka, na programu kama hizi zinahakikisha tunajenga rasilimali watu sahihi kufanikisha lengo hilo.”


Alibainisha kuwa serikali imeanzisha vifurushi vipya vya vivutio vya utalii, vikiwemo utalii wa chakula, ili kutangaza utajiri wa vyakula vya asili vya Tanzania:


Watalii wa leo wanatafuta uzoefu wa kweli. Sasa tunawaletea vyakula vya asili vya Kitanzania – ‘vyakula vya asili’ – kama sehemu ya vivutio vya utalii. Kutoka kwenye chakula safi, kisicho na kemikali moja kwa moja kutoka shambani, hadi vyakula vya kipekee vya mikoa mbalimbali, utalii wa chakula utawawezesha watalii kujifunza utamaduni wetu huku pia tukikuza uchumi wa jamii zetu,” alisema Waziri.


Aidha, Dkt. Chana alisisitiza kuwa utalii ni lazima uwe endelevu, shirikishi, na wenye manufaa kwa jamii, huku akipongeza ushirikiano kati ya SBL na NCT:


Ushirikiano huu ni mfano wa ubunifu tunaouhitaji – ambapo vijana wanapewa ujuzi siyo tu wa ajira, bali wa kujenga taaluma endelevu zinazoweka mbele maadili, utamaduni na huduma bora kwa watalii wetu.”


Mhe. Edward Mpogolo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, naye aliipongeza programu hiyo kwa kuchangia katika jitihada za serikali kukuza sekta ya utalii “Sekta ya utalii na ukarimu nchini Tanzania ina fursa kubwa ya kuzalisha ajira na kuchochea maendeleo ya taifa. Programu kama hii siyo tu kwamba inawapatia vijana wetu ujuzi, bali pia inasaidia kutekeleza dira ya serikali ya kugeuza utalii kuwa nguzo ya maendeleo jumuishi na endelevu. Nawapongeza SBL na NCT kwa dhamira yao ya kuwawezesha vijana wa Kitanzania kwa vitendo.”


Thursday, 15 May 2025

CRDB YAWAALIKA WANAHISA – MKUTANO MKUU WA 30 WA WANAHISA WAJA KWA KISHINDO!


Arusha, 14 Mei 2025: Benki ya CRDB imewataka wanahisa wake kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Mkutano Mkuu wa 30 wa Wanahisa, unaotarajiwa kufanyika Jumamosi, tarehe 17 Mei 2025, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya mafanikio tangu kuanzishwa kwa benki hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Hoteli ya Gran Meliá, jijini Arusha, ambapo Benki ya CRDB pia ilizindua Ripoti yake ya Mwaka 2024, inayoonyesha maendeleo makubwa ya kifedha, kiutendaji na kijamii yaliyopatikana katika kipindi hicho.



Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay, amesema kuwa Mkutano Mkuu wa mwaka huu utakuwa wa kipekee kwani utatanguliwa na semina maalum kwa wanahisa na umma, itakayofanyika Ijumaa, tarehe 16 Mei 2025, katika ukumbi wa Simba, AICC. “Semina hii ya kihistoria itakuwa chini ya kaulimbiu yetu ya mwaka huu: ‘Miaka 30 ya Ukuaji wa Pamoja,’ na itafunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango. Ni fursa muhimu ya kutafakari mafanikio yetu ya pamoja, changamoto tulizozishinda, na mwelekeo wetu wa miaka ijayo,” amesema Dkt. Laay.

Ajenda mbalimbali zitajadiliwa katika Mkutano Mkuu wa 30 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB ni pamoja na uchaguzi wa wajumbe wa bodi, kuteua wakaguzi wa hesabu, kujadili mapendekezo ya maboresho ya Katiba ya Benki, kujadili na kupokea Taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi, na Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa, pamoja na gawio kwa mwaka 2024 ambapo pendekezo la gawio la Sh 65 kwa hisa litawasilishwa.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa yamekamilika kwa asilimia 100. Nsekela amesema mkutano huo utafanyika kwa njia mseto “Hybrid Meeting” ili kutoa fursa kwa wanahisa wengi zaidi kushiriki moja kwa moja na kwa njia ya kidijitali. “Tumeweka muongozo wa jinsi ya kushiriki mkutano mkuu kwa njia ya mtandao kupitia tovuti yetu ya www.crdbbank.co.tz, mitandao yetu ya kijamii, lakini pia maelekezo yametumwa kwa ujumbe mfupi kwa Wanahisa,” amesema Nsekela huku akiwahakikishia kuwa Benki hiyo vizuri katika kuhakikisha wanashiriki bila chanagamoto yoyote.



Nsekela amewahamasisha wanahisa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Mkutano Mkuu huo wa kihistoria, akisisitiza kuwa uwepo wao ni muhimu kwa ajili ya kushuhudia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika miaka 30. “Tumejenga taasisi imara inayotoa huduma bora, tumeongeza thamani kwa wanahisa, na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa letu. Hii ni fursa adhimu kwa kila mwanahisa kujivunia sehemu yake katika mafanikio haya na kushiriki kuamua mustakabali wa benki yetu katika miaka ijayo,” amesisistiza.



Wednesday, 14 May 2025

TANZANIA HOSTS FIRST-EVER CUSTOMER EXPERIENCE CONFERENCE TO ADVANCE ECONOMIC AGENDA

Managing Director of Real Interactiv Inc. - Caroline Maajabu Mbaga, speaks to participants at the conference.

Historic gathering positions customer experience as key driver for Tanzania's economic transformation

Dar es Salaam, May 10, 2025: The inaugural Annual Customer Experience Conference, hosted by Real Interactiv Inc. in partnership with CX Academy Africa, successfully convened on May 9, 2025 at Hyatt Regency Hotel, sparking a transformative national conversation about customer experience as Tanzania's next economic frontier. The landmark event brought together more than 100 C-suite executives and public sector leaders from Tanzania's most influential organizations, including Vodacom, CRDB Bank, NBC Bank, Equity Bank, KCB, TANESCO, Helios, Strategis Insurance, Bumaco Insurance, Engie Mobisol, ZIC Takful and NSSF, to establish customer-centric strategies as fundamental to national growth.


The conference opened with powerful keynote addresses from globally recognized CX pioneers. Mandisa Makubalo, Founder and CEO of South Africa's Unlimited Experiences Group, captivated attendees with her presentation "The Voice of the Voiceless Customer," demonstrating how authentic customer understanding drives market leadership across African economies. Her insights were complemented by Jonathan Daniels, Managing Director of UK-based CX Centric, who delivered a compelling analysis of global customer-centricity trends and their specific applications for Tanzanian businesses seeking competitive advantage.


A conference highlight was CRDB Bank, Yolanda Uriyo, Head of Customer Experience as one of the sponsors, delivery of an inspiring keynote address titled "Customer Experience as Tanzania's Engine for Growth and Differentiation." With compelling examples from CRDB's transformation journey, Uriyo galvanized the audience by demonstrating how customer-centric strategies had directly contributed to the bank's market leadership and financial performance. "In today's competitive landscape, customer experience isn't just about satisfaction - it's our most powerful engine for sustainable growth and meaningful differentiation," Uriyo declared.


A pivotal moment occurred during the fireside chat "Customer Experience as a National Economic Catalyst," moderated by Caroline Maajabu Mbaga, Managing Director of Real Interactiv Inc. The discussion featured Tanzania Tourist Board Director General Ephraim Mafuru, who articulated how exceptional visitor experiences directly contribute to Tanzania's tourism sector, which accounts for nearly one-fifth of the nation's GDP. "Every interaction - from airport arrivals to hotel stays - represents either an opportunity to enhance Tanzania's global reputation or a risk to our economic potential," Mafuru emphasized. His perspective was reinforced by Felix John, Investment Promotion Manager at Tanzania Investment Center, who presented compelling data showing that investor decisions increasingly prioritize service quality alongside traditional economic factors.


The conference's practical sessions saw Tanzanian business leaders share real-world implementations of CX excellence. Vodacom's Customer Experience Operations Director Harriete Lwakatare and G4S Tanzania General Manager Imelda Lutebinga led an engaging panel on embedding customer-centric cultures within large organizations, while Dorothy Ndazi, Partner at Hilton Law Group, provided crucial guidance on balancing personalized experiences with data protection requirements.


David Makoha, Country Manager for IPSOS Tanzania, grounded the discussions in empirical evidence, presenting research demonstrating that Tanzanian companies with mature CX programs outperform sector averages by significant margins. These insights were put into practice during interactive workshops where cross-industry teams collaborated on customer journey mapping exercises under the guidance of international experts.


As the conference concluded, organizers announced several strategic initiatives to maintain momentum, including the establishment of annual Tanzania CX Innovation Awards and quarterly leadership roundtables. A complimentary resource toolkit, "50 Practical Ways to Elevate Customer Experience," was released to all attendees and made available for public download.