Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

Wednesday, 30 April 2025

BENKI YA CRDB YAPONGEZWA KWA USALAMA KAZINI



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete, ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa na mifumo bora ya usalama na afya ya wafanyakazi, wateja na jamii kwa ujumla mahala pa kazi.

Akizungumza katika kilele cha maonesho ya OSHA yaliyofanyika kitaifa mkoani Singida, Waziri Kikwete amesema: "Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inaamini kuwa usalama na afya mahali pa kazi ni haki ya msingi kwa kila mfanyakazi nchini, Benki ya CRDB imeonyesha mfano mzuri wa kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria ya Afya na Usalama Kazini ya mwaka 2003, nawapongeza sana, nampongeza pia Mkurugenzi Mtendaji wake ndugu yangu Abdulmajid Nsekela, hongereni sana Benki ya CRDB."

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, amesema Benki ya CRDB ni kati ya taasisi chache nchini zinazotekeleza kwa ufanisi kanuni za usalama kazini, na kusema ni taasisi bora inayoonyesha jinsi ya kuepuka majanga ya asili.

Meneja wa Afya na Usalama Kazini wa Benki ya CRDB, Salumu Shomali amesema: "Kila mwaka tunawafanyia uchunguzi wa afya wafanyakazi wetu uchunguzi wa afya wa kila mwaka na madaktari bingwa."



Katika maonesho hayo, amesema zaidi ya watu 400 walipata vipimo vya afya, na baadhi yao walipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kwa matibabu zaidi.

Katika maonesho hayo, Benki ya CRDB imeshinda tuzo ya mshindi wa tatu katika kipengele cha shughuli za fedha na bima katika kudumisha usalama wa wafanyakazi katika sekta ya fedha.



Meneja wa Afya na Usalama Kazini wa Benki ya CRDB, Salumu Shomali kwa pamoja na wafanyakazi wengine wa Benki ya CRDB wakiwa katika kilele cha maonesho ya OSHA yaliyofanyika kitaifa mkoani Singida.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete, akipokea zawadi wakati alipotembelea banda la Benki ya CRDB katika kilele cha maonesho ya OSHA yaliyofanyika kitaifa mkoani Singida

NMB YATAMBULIWA KWA UBORA KWENYE TUZO ZA OSHA 2025


Benki ya NMB imetunukiwa tuzo tano muhimu kutoka Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) katika Maadhimisho ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi kwa mwaka 2025, hatua inayodhihirisha juhudi za benki hiyo katika kuhakikisha mazingira salama na yenye afya kwa wafanyakazi wake.


Katika hafla hiyo iliyofanyika mkoani Singida, NMB ilitambuliwa kama Kampuni Bora kwenye Sekta ya Fedha na Bima kupitia Makao Makuu yake kwa kupata Tuzo ya Kwanza, na pia kutwaa Tuzo ya Pili kupitia Kanda ya Kati. Benki hiyo ilipata pia Tuzo ya Tatu kama Mshiriki Bora wa Maonesho ya OSHA, pamoja na Tuzo nyingine ya Tatu kwa kuwa Kampuni Iliyoibeba Vizuri Kaulimbiu ya Mwaka. Aidha, NMB ilipokea Tuzo Maalum ya Kutambuliwa kwa Mchango wake katika kufanikisha Maonesho ya OSHA 2025.


Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete, ambaye aliipongeza NMB pamoja na taasisi na makampuni mengine yaliyoshiriki. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Kikwete alisema kuwa Serikali itaendelea kuthamini na kuboresha mfumo wa utoaji tuzo za OSHA ili kuhamasisha uboreshaji wa usalama na afya katika maeneo ya kazi nchini.


Aidha, alizishukuru taasisi na kampuni zote zilizojitokeza kushiriki, akisisitiza kuwa ushiriki wao unaonesha utayari wa kupitia ukaguzi wa OSHA kama sehemu ya kuhakikisha viwango vya usalama na afya kazini vinazingatiwa.


Benki ya NMB iliwakilishwa na Meneja Mwandamizi wa Usalama Mahala pa Kazi, Abamwesiga Beneth, aliyefuatana na baadhi ya wafanyakazi kutoka matawi mbalimbali ya benki hiyo. Ushiriki na ushindi wa tuzo hizi ni ishara ya dhamira ya benki katika kuendeleza ustawi wa wafanyakazi wake na kuimarisha utamaduni wa usalama kazini.


HOW TECHNOLOGY IS TRANSFORMING TAX COLLECTION: THE CASE OF ETS IN TANZANIA


By Cynthia Bavo | Media and Tech Development Specialist

Taxes are a crucial source of revenue for governments. However, many Developing Countries struggle to collect sufficient revenues to finance the most basic of services such as healthcare and education, and finance investments in human capital and infrastructure, placing a disproportionate burden on citizens, particularly the poor. The World Bank estimates that 86% of low-income countries collect less than 15% of GDP in taxes, which is considered the minimum level of taxation that a country should collect to support its growth and development.

The Tanzanian Government has taken fundamental steps to make its tax system gain efficiency by leveraging technology, improve operational performance, enhance compliance, and support revenue collection, specifically through the Electronic Fiscal Devices (EFDs) and the Electronic Tax Stamp System (ETS). EFDs track sales transactions, ensuring proper reporting and compliance by businesses, while the ETS system monitors excisable goods such as tobacco, alcohol and spirits, beer, soft drinks, and water, preventing non-compliant manufacturers from evading taxes.

ETS is an instrument of compliance, as each stamp is proof that a producer or an importer is complying with its obligations to pay the excise duty tax set by the Government. The use of the ETS system is enforceable by the Electronic Tax Stamps Regulations (2018) and requires all manufactures and importers to be registered and to use it.

This move has helped the country to raise its tax collection by 81.6 percent, amassing an additional TZS 2,608 billion, compared to the pre-ETS era that was before 2019. Tax revenue collection in the fiscal year 2023/2024 increased by 18.1 percent compared to the previous fiscal year. From TZS 1.407 billion collected from ETS-marked products, TZS 1.007 billion came from excise duty alone.

Tuesday, 29 April 2025

BOLT LAUNCHES FLIGHT-TRACKING FEATURE IN TANZANIA TO ENHANCE AIRPORT PICKUPS

Dar es Salaam, 30 April 2025 - As technology and innovation continue to transform the finance and education sectors in Tanzania, the transport sector is also beginning to adopt digital changes aimed at increasing efficiency, speed, and convenience.

As of yesterday, taxi users can sync their flight details when scheduling a ride from the airport using the new Flight Tracking service in their Bolt app. If a customer’s flight is delayed or cancelled, Bolt will automatically adjust the pick-up time or cancel the trip at no extra cost.

To use the service, customers simply tap the ‘Schedule’ button in the Bolt app, enter Julius Nyerere International Airport as the starting point, and select their destination. Then they can tap ‘Add flight details’, enter the landing date, flight number, airline, or departure city, and choose their flight. Customers also choose how many minutes after landing they’d like to be picked up, and Bolt will handle any changes automatically in case of delays or cancellations.

Dimmy Kanyankole, General Manager of Bolt Tanzania and Kenya, said:

"Today, Bolt is an official ride-hailing partner of over 30 airports globally, including Dar es Salaam’s Julius Nyerere International Airport. This means customers can travel directly from Arrivals without needing to find a separate pick-up point. With the new Flight Tracking for Scheduled Rides option, both private and business customers can sync their flight details for seamless pick-up. If a flight is delayed or cancelled, the app adjusts the ride timing automatically — with no extra charge."

This is the latest upgrade to Bolt’s Scheduled Rides service since expanding the booking window to 90 days last year. According to the company, Tanzania’s market presents unique challenges that require tailored technology.

“For example, in France and Poland, customers can schedule ski shuttles for groups during ski season. In Cyprus, minibuses are used for tourist group trips,” added Dimmy.

TANZANIA YAJIPANGA KWA AJILI YA MKUTANO WA FUTURE READY NA WIKI YA UBUNIFU 2025

Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, Shigeki Komatsubara (katikati) akizungumza kwenye mdahalo uliofanyika wakati wa kutangaza msimu mpya wa Wiki ya Ubunifu sambamba na mkutano wa Future Ready Summit mwaka 2025. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire na muongozaji wa mdahalo huo Hilda Phoya.

Dar es Salaam – Ubunifu unachukua nafasi ya kipekee mwezi Mei wakati Tanzania ikijiandaa kwa ajili ya Wiki ya Ubunifu Tanzania maarufu kama ‘Innovation Week Tanzania(IWTz) kwa mwaka 2025, jukwaa shirikishi linaloangazia kuleta suluhisho kwa maendeleo endelevu.

Tukio hili litafanyika kuanzia tarehe 12 hadi 16 Mei 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), likiratibiwa kwa ushirikiano kati ya Vodacom Tanzania PLC, UNDP Tanzania kupitia programu yake ya FUNGUO na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH).

Ikiwa na kaulimbiu ya mwaka huu, "Ubunifu kwa Mustakabali Jumuishi na Wenye Ustahimilivu," IWTz 2025 inalenga kushughulikia changamoto kuu zinazolikumba taifa ikiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana, pengo la ujuzi wa kidijitali na maendeleo ya miji kwa kutumia nguvu ya ubunifu wa ndani ya nchi pamoja na mbinu bora za kimataifa. Mwaka huu pia, tukio hili litajumuisha Mkutano wa Vodacom Future Ready Summit (FRS2025), ambao utalenga mageuzi ya miji ya Tanzania kupitia ubunifu, miundombinu ya kidijitali na sera jumuishi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire, alisisitiza umuhimu wa maendeleo yanayoendeshwa na teknolojia na ushirikiano wa sekta mbalimbali: “Vodacom si mtoa huduma wa mawasiliano tu; sisi ni kichocheo cha maendeleo. Dhamira yetu ya kuendeleza ubunifu inaonekana katika kila mipango yetu — kutoka Code Like a Girl, Digital Accelerator hadi Future Ready Summit. Kupitia ushirikiano wetu na UNDP, COSTECH na wadau wengine, tunalenga kuchochea mijadala itakayounda Tanzania ijayo — Tanzania ya kidijitali, jumuishi na yenye ustahimilivu. Jukwaa hili linahusu kubadilisha mawazo na mitazamo, na kuwapa Watanzania zana za kuendesha mabadiliko ndani ya jamii zao.”

Kwa Vodacom, mkutano huu ni mwendelezo wa dhamira yake pana ya "kuunganisha watu kwa ajili ya mustakabali bora." Kupitia ubunifu kama vile M-Pesa, M-Pawa, VodaBima, M-Koba na majukwaa ya elimu ya kidijitali, kampuni hiyo imeonesha jinsi sekta binafsi inaweza kuongoza katika kutoa fursa sawa kwa wote.

MSHINDI WA KAMPENI YA TAP KIBINGWA AKABIDHIWA SUZUKI FRONX MPYA NA STANBIC

Mkuu wa Idara ya Wateja Maalum Benki ya Stanbic, Shangwe Kisanji (kulia) akimkabidhi kadi na funguo mshindi wa zawadi kuu ya kampeni ya TAP KIBINGWA Bw. Edwin Shayo baada ya kutangazwa kushinda kampeni hiyo . Kushoto ni Meneja wa Kadi Benki ya Stanbic, Irene Mutabihirwa.
  • Benki ya Stanbic na Visa wahitimisha kampeni hiyo nchi nzima kwa makabidhiano ya zawadi kuu jijini Dar es Salaam
  • Edwin Shayo anyakua gari ya kifahari Suzuki Fronx baada ya miezi mitatu ya zawadi za kidijitali
  • Zaidi ya asilimia 80% ya wateja wanaohusika, TZS 7.5 milioni zilizotolewa kama zawadi ya fedha taslimu, na matumizi ya kadi za kidijitali kupanda kwa asilimia 20%
Dar es Salaam, Aprili 24, 2025: Benki ya Stanbic Tanzania, kwa kushirikiana na Visa, wamekamilisha fainali yake ya Kampeni ya Tap Kibingwa kwa mafanikio makubwa kwa kumkabidhi rasmi mshindi wa zawadi kuu ya Suzuki Fronx, Edwin Shayo. Makabidhiano hayo yalifanyika katika eneo la kazi la mshindi huyo Mikocheni, huku ukiongozwa na msafara uliopambwa na chapa ya Stanbic kutoka makao makuu—wakisherehekea sio tu kwa kupata mshindi bali mabadiliko makubwa katika jinsi Watanzania wanavyojihusisha na benki kidijitali.


Kampeni ya Tap Kibingwa ilianza Januari hadi Aprili 2025, ikiwa na dhamira ya wazi: kutumia miamala bila pesa taslimu na kuzawadia wateja ambao walitumia kikamilifu Kadi zao za Debit za Visa kwa malipo ya kila siku. Kupitia mpango huu, Benki ya Stanbic iliimarisha jukumu lake kama kichocheo cha ujumuishaji wa kifedha, uvumbuzi wa malipo, na suluhisho za kibenki zinazozingatia wateja.


"Tap Kibingwa ilikuwa zaidi ya kampeni-ilikuwa harakati ya kuwasaidia Watanzania kupata urahisi na usalama wa malipo ya kidijitali," alisema Shangwe Kisanji, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya Stanbic Tanzania. "Leo tunasherehekea sio tu ushindi wa Edwin lakini maelfu ya wateja waliochagua kutumia huduma ya kidijitali mara kwa mara na bila kusita."


Katika muda wote wa kampeni, Stanbic ilitoa droo tatu za kila mwezi, kila moja ikiwazawadia wateja watano TZS 500,000. Kwa jumla, wateja 15 walipata TZS 7.5 milioni kama zawadi ya fedha taslimu. Matarajio yaliongezeka, huku zaidi ya asilimia 80% ya wateja wakishiriki na ongezeko la asilimia 20% la matumizi ya Visa Debit Card kwa wateja wa Stanbic.


Kivutio kikuu cha kampeni hiyo kilikuwa ni makabidhiano ya Suzuki Fronx ya mwaka 2024 yenye matumizi ya umbali usiozidi maili sifuri, alizawadiwa Edwin Shayo kwa kushinda katika droo kuu kupitia matumizi yake ya mara kwa mara ya kadi ya thamani ya juu.


"Kushinda gari hili ni baraka, na ninaishukuru Stanbic kwa mpango huu wa kipekee," alisema Edwin Shayo. "Zaidi ya kila kitu kwa sasa naona umuhimu wa kutokuwa na pesa taslimu. Ni matumizi ya Visa ambayo ni ya haraka, salama, na rahisi zaidi."


Kampeni hii inawiana kwa karibu na agizo la Benki Kuu la Tanzania la kupanua upatikanaji wa huduma za kifedha za kidijitali na kupunguza utegemezi wa fedha taslimu, hasa wakati taifa linavyozidi kushika kasi kuelekea uchumi shirikishi na unaoendeshwa na teknolojia.

Monday, 28 April 2025

GEITA GOLD MINING LAUNCHES KILI CHALLENGE 2025 TO SUPPORT HIV/AIDS FIGHT

The Minister for Communication and Information Technology, Hon. Jerry William Silaa, speaks in Dar es Salaam over the weekend, during the official launch of the GGM Kili Challenge 2025 campaign, which involves climbing Mount Kilimanjaro to raise funds in support of the fight against HIV/AIDS. The campaign is held under the main sponsorship of Geita Gold Mining Limited (GGML).
Senior Manager for Sustainability at Geita Gold Mining Limited (GGML), Mr. Gilbert Mworia, speaks in Dar es Salaam over the weekend, during the official launch of the GGM Kili Challenge 2025 campaign.

Geita Gold Mining Limited (GGML) has officially launched the Kili Challenge 2025, a major fundraising initiative aimed at supporting the national response to HIV/AIDS, the campaign, organized in partnership with the Tanzania Commission for AIDS (TACAIDS), seeks to mobilize domestic resources to fund HIV/AIDS prevention, treatment, and care efforts across the country.



Speaking during the launch event in Dar es Salaam, during the weekend, the Minister for Communication and Information Technology, Hon. Jerry William Silaa, applauded GGML and TACAIDS for their continued collaboration, noting that since its inception in 2002, the Kili Challenge has been a vital platform for raising funds to support HIV/AIDS services.



“This campaign is not just about fundraising. It is about uniting efforts to reduce HIV-related stigma, enhance access to treatment, and support vulnerable communities,” said Minister Silaa.



He further emphasized the government’s commitment under the leadership of President Dr. Samia Suluhu Hassan to eliminate HIV/AIDS in Tanzania by 2030, citing significant progress made under the Sixth Phase Government.



According to statistics the Minister said, the number of new HIV infections in Tanzania has dropped from 72,000 annually (2016–2017) to 60,000 annually (2022–2023), demonstrating the impact of the country's interventions, however, he noted that as of December 2024, an estimated 1.7 million Tanzanians are living with HIV, with over 1.5 million already accessing antiretroviral therapy (ART).



The Kili Challenge 2025 invites individuals from all sectors to participate in a fundraising event that will involve climbing and cycling around Mount Kilimanjaro, the farewell ceremony for participants will take place on July 18, 2025, followed by a welcome ceremony on July 24, 2025, in Kilimanjaro Region.



Over the past two decades, the Kili Challenge has raised millions of dollars for HIV/AIDS initiatives, particularly benefiting people living with HIV, orphans, and marginalized communities, this year’s proceeds will fund HIV prevention programs, treatment services, and economic empowerment initiatives for high-risk groups.



Speaking on behalf of GGML Managing Director Duran Archery, the company's Senior Manager for Sustainability, Gilbert Mworia, reiterated GGML's commitment as the event’s main sponsor.

BENKI YA DUNIA YAIMWAGIA SIFA TANZANIA KWA KUSIMAMIA VIZURI UCHUMI WAKE

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kulia), akiwa na Makamu mpya wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiamé Diop, walipokutana na kufanya mazungumzo kwenye Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kushoto), ukiwa katika mazungumzo na Timu ya Benki ya Dunia ikiongozwa na Makamu mpya wa Rais wa Benki hiyo anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiamé Diop, kwenye Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.

Na Benny Mwaipaja, Washington D.C, Marekani

Benki ya Dunia imeimwagia sifa Tanzania kwa usimamizi mzuri wa uchumi wa nchi na kuwa nchi ya kupigiwa mfano barani Afrika licha ya misukosuko mbalimbali ya kiuchumi inayoikabili dunia.



Pongezi hizo zimetolewa na Makamu mpya wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiamé Diop, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania, unaoongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, kwenye Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.



Dkt. Diop alisema kuwa Tanzania ni nchi ya mfano katika usimamizi wa sera za uchumi na fedha ambapo licha ya changamoto za UVIKO 19 na mizozo ya kisiasa inayoendelea sehemu mbalimbali duniani, tathimini ya Benki hiyo inaonesha kuwa uchumi wa Tanzania uko imara ikilinganishwa na nchi nyingine nyingi za Afrika.



Alisifu pia mikakati iliyowekwa na Serikali kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya Sera za nje za Marekani na duniani kwa ujumla za kupunguza misaada na kuondoa ufadhili katika miradi mbalimbali ikiwemo sekta ya afya, kwa kutumia fedha zake za ndani.



Aidha, alipongeza uhusiano imara uliopo kati ya Tanzania na Benki ya Dunia na kuahidi kuwa Benki yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kukuza uchumi na kuwaondolea umasikini wananchi wake kwa kusaidia fedha zitakazotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii pamoja na kutoa misaada ya kiufundi itakayochochea ukuaji wa uchumi.



Kwa upande wake, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alimweleza Makamu mpya wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiamé Diop, aliyechukua nafasi ya Bi. Victoria Kwakwa, aliyemaliza muda wake, kwamba Benki ya Dunia ni mdau mkubwa wa maendeleo wa Tanzania.

NCBA BANK PLANTS 5,000 TREES TO RESTORE MPIJI RIVERBANK IN BUNJU B, DAR ES SALAAM

NCBA Bank Acting Managing Director, Alex Mziray.

25 April 2025 - In a bold demonstration of corporate environmental responsibility, NCBA Bank Tanzania led a major tree-planting initiative along River Mpiji in Bunju B, Dar es Salaam. The campaign involved the planting of 5,000 trees and was attended by the Bank’s Acting Managing Director, Mr. Alex Mziray, alongside regional government officials, community leaders and environmental stakeholders.


River Mpiji, a key waterway in Kinondoni District, has for years suffered from environmental degradation caused by deforestation, waste dumping, informal settlement growth, and unchecked urban expansion. The result has been eroded riverbanks, reduced water quality, and compromised biodiversity. Recognizing the ecological urgency, NCBA Bank took a proactive step with this intervention to help rehabilitate the river’s fragile ecosystem and safeguard it for future generations.


Speaking at the event, Mr. Mziray emphasized that the Bank’s commitment to sustainability goes beyond rhetoric:

We believe in acting with purpose. By planting these 5,000 trees, we are helping to rebuild a critical water ecosystem, fortify community resilience, and underscore the role the private sector must play in climate action. It is not enough to talk about sustainability we must live it.”


The initiative aligns with NCBA’s broader environmental goal of planting over 10,000 trees nationwide by the end of 2025, a target the Bank is steadily pursuing. Prior campaigns have already seen trees planted in Zanzibar, Arusha, Mwanza, and Dar es Salaam’s Jangwani area, each designed to address different ecological needs coastal erosion, urban green cover, and hospital-area beautification and resilience.


The planting in Bunju B included indigenous and climate-resilient species chosen specifically for their ability to stabilize soil, absorb excess water, and support the native flora and fauna. Experts on-site also trained volunteers on how to care for the trees after planting, ensuring the effort results in long-term survival and growth.


What set this campaign apart was the deep community involvement. Over 300 participants, including schoolchildren, local residents, and environmental clubs, were actively involved in the day’s activities. “This is not just an event. It is a movement,” said one community elder. “We now feel responsible for protecting this river.

Sunday, 27 April 2025

NMB YADHAMINI BONANZA LA WIKI YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI



Katika kuadhimisha Wiki ya Maonesho ya Kitaifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, Benki ya NMB imedhamini na kushiriki bonanza maalum lililoandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) mjini Singida.

Bonanza hilo, lililofanyika katika Uwanja wa VETA - Singida, lilikutanisha makampuni kutoka sekta binafsi na ya umma yaliyoshindana katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete na kuvuta kamba, likiwa na lengo la kuhimiza afya na usalama kazini kupitia michezo.



Mgeni rasmi katika hafla hii alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, ambaye aliipongeza Benki ya NMB kwa mchango wake mkubwa katika kufanikisha tukio hilo muhimu. Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mhe. Dendego alisisitiza umuhimu wa mazoezi katika kuboresha afya za wafanyakazi, akieleza kuwa ustawi wa wafanyakazi ni msingi wa uzalishaji bora na maendeleo ya taifa.



Kauli mbiu ya mwaka huu katika Wiki ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ni “Nafasi ya Akili Mnemba na Teknolojia za Kidijitali katika Kuimarisha Usalama na Afya Mahali Pa Kazi,” ikilenga kuhimiza matumizi ya teknolojia na ubunifu wa kidijitali katika kulinda afya na usalama wa wafanyakazi.



Mbali na kushiriki katika bonanza, Benki ya NMB pia imeweka banda maalum katika Viwanja vya Maonesho vya Mandewa ambapo wananchi wanapata fursa ya kujifunza namna benki hiyo inavyohakikisha usalama mahali pa kazi, pamoja na kupata elimu ya kifedha na huduma nyingine za kibenki.



Benki ya NMB inajivunia kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kuimarisha afya na usalama wa wafanyakazi nchini, ikiendelea kushirikiana na taasisi za umma na binafsi katika kujenga mazingira bora ya kazi.