Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Friday, 12 December 2025

VODACOM YAENDELEA KUSAMBAZA MAKAPU YA SIKUKUU, SAFARI YAINGIA SOKO LA MACHINGA DODOMA

Katika muendelezo wa kampeni yake ya kusambaza Kapu la Vodacom katika maeneo mbalimbali nchini, timu ya Vodacom Tanzania Plc imefika katika Soko la Machinga jijini Dodoma na kuwapatia wateja wake makapu maalum yaliyosheheni bidhaa mbalimbali kwa ajili ya msimu wa sikukuu.

Zoezi hili ni sehemu ya mwendelezo wa utoaji wa makapu ambao tayari umetekelezwa katika mikoa mingine nchini, likilenga kuwafikia wateja wengi zaidi na kusherehekea nao katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka. Kupitia hatua hii, Vodacom inaonyesha utayari wake wa kurudisha shukrani kwa wateja wanaoendelea kuiamini na kutumia huduma zake kila siku.

Mbali na kuwa sehemu ya kusherehekea msimu wa sikukuu, kampeni hii pia inahitimisha maadhimisho ya miaka 25 ya Vodacom tangu ilipoanza kutoa huduma nchini Tanzania. Kwa muda wote huo, kampuni imeendelea kujidhihirisha kama miongozo ya ubunifu na suluhisho za kidijitali zinazowawezesha Watanzania kuwasiliana, kufanya biashara, na kufikia fursa mbalimbali kwa urahisi zaidi.

Vodacom inaendelea kutoa wito kwa wateja wake kufuatilia ziara hizi za ugawaji makapu katika maeneo mengine ili nao wawe miongoni mwa watakaonufaika na zawadi hizi katika msimu huu wa furaha.

No comments:

Post a Comment