Vodacom Tanzania imeendelea kuunganisha wateja wake na furaha za msimu wa sikukuu kupitia zoezi la kugawa makapu maalum ya zawadi. Mwishoni mwa wiki mjini Morogoro, Mkuu wa Kanda ya Kati, Chiha Nchimbi (kushoto), akiwa pamoja na Meneja Mauzo na Mkakati wa Biashara wa Kanda hiyo, Latifa Salum (kulia), walimkabidhi kapu la sikukuu mteja Beatrice Msawanya (katikati) kama ishara ya kuthamini uaminifu na uhusiano mzuri uliopo kati ya kampuni na wateja wake.
Utoaji huu ni sehemu ya kampeni inayoendelea ya Vodacom ya kuwashukuru na kusherehekea wateja wake nchini kote katika kipindi hiki cha sikukuu. Kupitia kampeni hii, Vodacom inaendelea kujenga ukaribu na jamii huku ikichochea furaha na mshikamano katika msimu huu maalum.

.jpeg)
.jpeg)


No comments:
Post a Comment