Dar es Salaam, 10 Septemba 2025 – Ecobank, benki inayoongoza barani Afrika, inasherehekea miaka 40 ya huduma bora Afrika na miaka 15 ya huduma nchini Tanzania. Katika maadhimisho haya, Ecobank imezindua kampeni kabambe ya “Gutuka na Ecobank!” yenye lengo la kuhamasisha tabia ya kuweka akiba na kuwashukuru wateja kwa uaminifu wao.
KUHUSU KAMPENI
Kampeni hii ya miezi mitatu inalenga wateja wa akaunti ya Supa Seva, ambapo watapata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali.
Akizungumza kwenye uzinduzi, Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Innocent Urio, alisema:
“Kupitia kampeni hii, wateja wetu watajipatia zawadi mbalimbali zikiwemo pikipiki za miguu mitatu (Gutas) na pesa taslimu hadi TZS 1,000,000. Mwishoni mwa kampeni, zawadi kubwa itakuwa GUTA (Tricycle) kupitia droo ya bahati nasibu.”
JINSI YA KUSHIRIKI
- Fungua akaunti ya Supa Seva kupitia www.ecobank.com au tawi lolote la Ecobank.
- Weka akiba kwenye akaunti yako – kadri unavyoongeza akiba, ndivyo nafasi zako za ushindi zinavyoongezeka.
FAIDA ZA AKAUNTI YA SUPA SEVA
- Hakuna makato ya kila mwezi.
- Riba nono hadi 5% inayolipwa kila robo mwaka.
- Utoaji wa bure mara moja kwa mwezi kupitia matawi yote ya Ecobank.
- Huduma ya Lipa Namba bure kwa wateja wa SMEs (inahudumia malipo kutoka benki zote na mitandao ya simu).
- Riba inaendelea kulipwa hata baada ya kampeni kuisha.
KAULI YA UONGOZI
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Wakati (SME), Juma Hamisi, alisema:
“Gutuka na Ecobank sio tu kampeni ya zawadi, bali ni sehemu ya maadhimisho ya safari yetu ya miaka 40 barani Afrika na miaka 15 nchini Tanzania. Ni zawadi kwa wateja wetu kwa uaminifu wao, na pia ni hatua ya kujenga utamaduni wa kuweka akiba kwa maisha bora ya kifedha.”
WITO KWA WATEJA
Ecobank inawaalika Watanzania wote kushiriki kwenye kampeni hii na kufurahia zawadi kemkem. Kwa maelezo zaidi:
📞 Piga bure: 0800 110 021
🏦 Tembelea matawi yetu: Dar es Salaam, Arusha na Mwanza
🌐 Fuata kurasa za Ecobank kwenye mitandao ya kijamii
Gutuka na Ecobank – Akiba Zaidi, Ushindi Zaidi!



No comments:
Post a Comment