Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Monday, 18 August 2025

NMB ‘YAWAPIGA MSASA’ WAZAZI, WALEZI WA WANAFUNZI AL-RAHMAH COMPLEX

Na Mwandishi Wetu, Mkuranga

Kuelekea Mitihani ya Taifa ya mwisho wa mwaka kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, Benki ya NMB imewataka wazazi na walezi kujenga msingi imara wa maisha bora ya watoto wao kwa kuwazoesha utamaduni chanya wa kuweka akiba kwa ajili ya maendeleo ya kielimu na kimaisha.

Wito huo ulitolewa na Meneja wa NMB Tawi la Mkuranga, Godwin Manimo, katika mahafali ya tatu na ya tano ya wanafunzi wa Kidato cha Nne na Darasa la Saba wa shule za Al-Rahmah Complex, yaliyofanyika Mkuranga mkoani Pwani chini ya usimamizi wa Al-Rahmah Development Complex.

Mitihani ya Taifa ya Darasa la Saba, inayoandaliwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), imepangwa kufanyika Septemba 10 na 11 mwaka huu, huku ile ya Kidato cha Nne ikianza Novemba 10, 2025. Wanafunzi wa Al-Rahmah wataungana na wenzao kote nchini kuhitimisha hatua moja ya elimu kabla ya kuanza nyingine mwaka 2026.

Akizungumza katika mahafali hayo yaliyodhaminiwa na NMB kupitia Akaunti za Mtoto na Chipukizi, Manimo aliwapongeza wazazi na walezi kwa kujitoa na kuwekeza katika elimu ya watoto wao.

“NMB tumedhamini mahafali haya kama ishara ya kuunga mkono juhudi za Al-Rahmah Complex na walimu wake, ambao wanawajengea watoto msingi imara wa maarifa na maadili. Pamoja na hilo, tumekuja na suluhisho la kifedha kwa ajili ya watoto – akaunti mbili rafiki, NMB Mtoto Account na NMB Chipukizi Account, ambazo zitawasaidia wazazi kuweka akiba mapema kwa ajili ya mahitaji ya elimu na maendeleo ya baadaye,” alisema Manimo.

Katika kuunga mkono juhudi hizo, NMB ilifungua akaunti kwa wanafunzi 10 walioongoza kwa ufaulu (Top 5 Darasa la Saba na Top 5 Kidato cha Nne), kila mmoja akiwekewa akiba ya Sh80,000. Aidha, wanafunzi 64 wa kwanza walipewa akaunti za bure na kuwekewa Sh10,000 kila mmoja.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Al-Rahmah Complex, Dk. Ally Abdulgaffar, aliahidi maboresho makubwa kwa shule hizo ikiwemo:

  1. Kuanzisha mafunzo ya awali ya Teknolojia ya Akili Bandia (AI) kuanzia mwaka 2026 kwa wanafunzi wa pre-form one.
  2. Kuanzisha Programu ya Mabalozi wa Al-Rahmah kwa wahitimu wa Kidato cha Nne na Sita, watakaotangaza maadili na mafanikio ya shule hizo katika jamii.
  3. Kuzindua Leadership Programme ili kuwajengea wanafunzi ujuzi wa uongozi watakapomaliza masomo yao.

Omary Said Msumba, Mtakwimu kutoka NECTA na mgeni rasmi, alipongeza hatua hizo na kueleza kuwa kuingiza somo la AI mapema shuleni ni hatua kubwa inayowafanya Al-Rahmah kuwa kielelezo kwa taifa.

“Artificial Intelligence ni hot cake. Either you go with it or you die. Haiwezekani kufanikisha maendeleo bila AI. Hongereni kwa kuwa mbele ya wakati, hata kabla ya Serikali kuanzisha rasmi,” alisema Msumba.

Katika risala ya wanafunzi, iliyosomwa na Faiz Abdulmalick Feruzi, waliishukuru NMB kwa udhamini na kuomba msaada wa kushughulikia changamoto za makazi ya walimu, viwanja vya michezo, vifaa vya kujifunzia na ufadhili wa vipaji maalum vya wanafunzi.









No comments:

Post a Comment