Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Thursday, 21 August 2025

EQUITY BANK YACHANGIA MADAWATI 100 SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA NYANKUMBU – GEITA

Geita – Serikali wilayani Geita imezitaka taasisi mbalimbali nchini kuendelea kujitolea kusaidia sekta ya elimu kama njia ya kuchangia maendeleo ya taifa.

Akizungumza wakati wa kupokea msaada wa madawati 100 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 yaliyotolewa na Equity Bank Tanzania kwa Shule ya Sekondari ya Wasichana Nyankumbu, Afisa Tarafa wa Wilaya ya Geita Moreen Komanya alisema hatua hiyo inaunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita.

“Tunazihimiza taasisi nyingine pia zione umuhimu wa kusaidia sekta ya elimu kwa kuwa ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa letu,” alisema Komanya.

 

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Kitengo cha Biashara cha Equity Bank Tanzania Leah Ayoub alisema benki hiyo imekuwa ikijikita katika kuunga mkono jamii kwa maendeleo endelevu sambamba na huduma za kifedha.

“Mbali na msaada huu, tumezindua pia tawi jipya la benki mjini Geita ili kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha na kuhakikisha ujumuishaji wa kifedha unakuwa na manufaa kwa jamii yote ya Watanzania,” alisema Ayoub.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Khadija Kayanda, aliishukuru benki kwa mchango huo akibainisha kuwa utaboresha mazingira ya kujifunza na kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Nao wanafunzi wa shule hiyo akiwemo Agripina Elisha na Hilda Baton Sanga waliishukuru Equity Bank kwa msaada huo na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano huo.

“Tunafurahi kuona taasisi za kifedha kama Equity si tu zinatoa huduma za kifedha bali pia zinaguswa na maendeleo ya elimu na jamii kwa ujumla,” alisema Agripina.





No comments:

Post a Comment