Mkata, Handeni Vijijini — 5 Julai 2025
Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa Vodacom Tanzania PLC, George Venanty (pichani kushoto), amemkabidhi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mkata kiti cha ulemavu ikiwa ni sehemu ya msaada mkubwa uliotolewa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Benki ya Stanbic Tanzania kupitia msafara wa Twende Butiama.
Katika hafla hiyo, shule imenufaika kwa kupokea:
- Matundu ya choo 10,
- Vitanda 20,
- Magodoro 40, na
- Viti maalum 47 vya walemavu.
Msaada huo unalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi, hasa wale wenye mahitaji maalum, ikiwa ni sehemu ya dhamira ya Vodacom na Stanbic katika kusaidia maendeleo ya elimu na ustawi wa jamii.
Aidha, kama sehemu ya juhudi za kulinda mazingira, msafara huo uliweza kupanda miti 100 katika kata ya Mkata, Wilaya ya Handeni Vijijini, Mkoa wa Tanga.
Msafara wa Twende Butiama, ulioanza rasmi Julai 3, 2025, unaendelea kupitia maeneo mbalimbali ya Tanzania ukiwa na lengo la kuhimiza mshikamano wa kitaifa, utunzaji wa mazingira, na kuchochea maendeleo ya kijamii kupitia miradi ya kijamii na misaada ya kijamii yenye tija.
No comments:
Post a Comment