Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Monday, 30 June 2025

VODACOM NA STANBIC WAZINDUA JEZI RASMI YA MSAFARA WA TWENDE BUTIAMA 2025

Dar es Salaam, Juni 28, 2025 – Kampuni ya Vodacom Tanzania, kwa kushirikiana na Benki ya Stanbic, imezindua rasmi jezi itakayotumika katika msafara wa Twende Butiama 2025 – tukio maalum la waendesha baiskeli linalolenga kuchochea maendeleo ya kijamii kupitia sekta za elimu, afya na mazingira.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire, alisema kuwa ushirikiano kati ya kampuni hiyo na Benki ya Stanbic ni sehemu ya dhamira ya kuenzi mchango wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kupitia vitendo vya kijamii vinavyolenga kuboresha maisha ya Watanzania.

“Katika kumuenzi Baba wa Taifa kwa vitendo, sisi Vodacom Tanzania tunaungana na jamii kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo – ikiwemo afya, elimu, na utunzaji wa mazingira,” alisema Besiimire.


STANBIC YADHAMIRIA KUCHANGIA TZS MILIONI 100 KILA MWAKA

Kwa upande wake, Wilmot Ishengoma, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Stanbic Bank, Manzi Rwegasira, alieleza kuwa benki hiyo imeguswa na mafanikio ya msafara huo katika miaka iliyopita, na hivyo kujitolea kuchangia shilingi milioni 100 kila mwaka kuunga mkono juhudi hizi.

“Tanzania ni nyumbani. Maendeleo na ukuaji wake ni jukumu letu sote. Ili kushinda maadui watatu wa maendeleo – ujinga, umaskini, na maradhi – tumeona umuhimu wa kushiriki kikamilifu msafara huu. Tutaendelea kuchangia shilingi milioni 100 kila mwaka ili kuhakikisha msafara huu unaendelea kuleta mafanikio kwa jamii,” alisema Ishengoma.


TWENDE BUTIAMA 2025: MAPAMBANO DHIDI YA MAADUI WA MAENDELEO

Kaulimbiu ya msafara wa mwaka huu ni:
“Kupambana na Maadui Watatu wa Maendeleo: Ujinga, Umaskini na Maradhi.”

Msafara wa Twende Butiama unatarajiwa kuvutia washiriki kutoka nchi mbalimbali ikiwemo:
🇰🇪 Kenya, 🇺🇬 Uganda, 🇷🇼 Rwanda, 🇧🇮 Burundi, 🇨🇩 Congo, 🇿🇲 Zambia, 🇲🇼 Malawi, 🇳🇬 Nigeria, na hata 🇺🇸 Marekani.


KUHUSU MSAFARA WA TWENDE BUTIAMA

Msafara wa Twende Butiama ni kampeni ya kipekee inayowakutanisha waendesha baiskeli kutoka mataifa mbalimbali kwa lengo la kuchochea hamasa ya maendeleo ya kijamii kwa njia ya ushiriki wa moja kwa moja katika miradi ya afya, elimu, na mazingira. Msafara huu pia hutumika kama jukwaa la kushirikisha wadau wa maendeleo katika kuchangia jamii kwa vitendo.

No comments:

Post a Comment