Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Monday, 23 June 2025

ACCESS BANK YAKAMILISHA UNUNUZI WA HUDUMA ZA KIBINAFSI NA BIASHARA ZA STANDARD CHARTERED

Mkurugenzi Mtendaji wa Access Bank, Imani John (kushoto) na Herman Kasekende kutoka Benki ya Standard Chartered wakibadilishana nyaraka za ununuzi wa Kitengo cha Huduma za Wateja wa Kawaida, Binafsi na Biashara cha Benki ya Standard Chartered Tanzania, baada ya kukamilika kwa taratibu zote muhimu za kisheria na kupokelewa kwa idhini kutoka kwa mamlaka husika za udhibiti.

Benki ya Access Tanzania yapanua huduma zake nchini, yaimarisha huduma za kibinafsi na biashara, na kuchochea ujumuishaji wa kifedha kwa Watanzania wote.

Dar es Salaam, 23 Juni 2025 – Access Bank Tanzania leo imetangaza rasmi kukamilika kwa mafanikio ya ununuzi wa kitengo cha Huduma za Wateja wa Kawaida, Binafsi na Biashara cha Benki ya Standard Chartered Tanzania, baada ya kukamilika kwa taratibu zote muhimu za kisheria na kupokelewa kwa idhini kutoka kwa mamlaka husika za udhibiti.

Hatua hii inaashiria mafanikio makubwa katika safari ya mageuzi ya Access Bank Tanzania kama benki ya biashara kamili inayolenga utoaji wa huduma jumuishi, salama, na za kidijitali kwa watu binafsi, wajasiriamali, na wafanyabiashara nchini kote.



Ununuzi huu hauhusiani tu na upanuzi wa huduma bali ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yetu ya kuwafikia Watanzania wengi zaidi kwa huduma za kibenki za kiwango cha kimataifa zinazoweka mteja mbele,” alisema Imani John, Mkurugenzi Mtendaji wa Access Bank Tanzania.

Kwa kuchanganya uzoefu wa Standard Chartered katika huduma za kifedha na mtazamo wa kidijitali unaoongozwa na Access Bank pamoja na mtandao wetu barani Afrika, tunajenga jukwaa madhubuti la uwezeshaji wa kifedha kwa wote.”

Kupitia ununuzi huu, Access Bank Tanzania imeongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wake wa kuwahudumia Watanzania, na kuchangia kwa dhati ajenda ya taifa ya ujumuishaji wa kifedha. Benki sasa itaweza kutoa huduma zilizobuniwa mahsusi kulingana na mahitaji ya makundi mbalimbali ya jamii, yakiwemo watu wasiokuwa na akaunti benki, wenye kipato kikubwa, wamiliki wa biashara ndogo na za kati Akaunti za Biashara, wanawake na vijana.

Faida Kuu za Ununuzi Huu:

Huduma Pana na Shirikishi

Wateja watapata huduma mbalimbali za kifedha kwa mtu binafsi na biashara, zikiwemo akaunti za akiba na mikopo, huduma za kidijitali, mikopo ya biashara, huduma za uwekezaji, na huduma za biashara za kimataifa.

Huduma Maalum kwa Wateja wa Thamani ya Juu

Benki sasa inatoa huduma zilizoboreshwa kwa wateja binafsi wa kipato cha juu, zikiwemo usimamizi wa mali (wealth management), uwekezaji katika sarafu mbalimbali, na huduma binafsi za usimamizi wa uhusiano. Wateja pia watanufaika na huduma za kuvuka mipaka kupitia mtandao wa Access Bank katika masoko 24 duniani.

Kuwezesha Biashara Ndogo na za Kati (Akaunti za Biashara)

Kupitia jukwaa la PrimusPlus, Access Bank inapanua huduma za benki kwa Akaunti za Biashara, ikiwa ni pamoja na mikopo maalum, suluhisho za mtaji wa kazi, ushauri wa kifedha, na elimu ya fedha kwa ajili ya ukuaji wa biashara na kuunganika na minyororo ya thamani ya kikanda.

Kuinua Wanawake Kiuchumi

Kupitia mpango huo, benki imejipanga kuwawezesha wanawake kupitia mikopo ya malengo maalum, mafunzo ya ujasiriamali, na fursa za upatikanaji wa masoko kwa ajili ya kukuza biashara zao katika kila hatua.

Uzoefu Bora kwa Mteja

Mpito huu umeandaliwa kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha huduma kwa wateja zinaendelea kwa ubora uleule au zaidi, kwa kutumia timu maalum za mahusiano na njia bora za mawasiliano.

Kuendeleza Ubunifu

Access Bank inaendelea kuboresha huduma zake za kidijitali kupitia majukwaa kama AccessMore App, huduma za USSD, na PrimusPlus kwa wateja wa biashara – yote haya yakilenga kufanya huduma za benki kuwa rahisi, haraka, salama na jumuishi zaidi.

Uchumi wa Tanzania una nguvu kubwa, lakini bado kuna Watanzania wengi ambao hawajafikiwa na huduma rasmi za kifedha,” alisema Bi. John.

Muunganiko huu unatuwezesha kuwahudumia wateja wetu kwa ufanisi zaidi na kuwapa suluhisho ambazo si tu zinapatikana, bali pia zinawezesha.”

Tunawakaribisha kwa moyo wote wateja wetu wapya kwenye familia ya Access Bank. Pamoja, tutaijenga Tanzania yenye ustawi wa kifedha kwa wote.”

No comments:

Post a Comment