Katika kuadhimisha Wiki ya Usalama Barabarani Duniani (May 12 - 18, 2025), kampuni ya Puma Energy Tanzania kwa kushirikiana na shirika la Amend Tanzania wameendesha 'Mahakama Kifani ya Watoto' kuhusu usalama barabarani tukio ambalo ni sehemu muhimu ya programu ya kampeni ya elimu ya usalama barabarani kwa shule za msingi ambayo pia inajulikana kama ‘Be Road Safe Africa’. Tukio hilo lilifanyika katika Shule ya Msingi ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, kuanzia mwanzoni mwa wiki na kuhitimisha siku ya Ijumaa ya Mei 16.

No comments:
Post a Comment