- Yasisitiza dhamira yake kukuza uzalishaji mazao ya kilimo
Akizungumzia kampeni hiyo ya miezi miwili Bw Urassa alisema inatoa fursa kwa wakulima wa zao la ufuta mkoa wa Lindi na Wilaya za Masasi na Nanyumbu mkoani Mtwara kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo pikipiki na kompyuta mpakato ‘Laptops’, huku akitaja kuwa walengwa ni wakulima wa zao la ufuta kupitia vyama vya msingi, vyama vikuu vya ushirika na mkulima mmoja mmoja ambao wanahudumiwa na benki hiyo.
“Lengo la kampeni hii ni kuwahamasisha wakulima wa zao la ufuta kwenye mkoa wa Lindi na Mtwara kutunza fedha zao kwenye mifumo rasmi ya kifedha hasa benki badala ya kutunza kwenye mifumo isiyo rasmi. Tunawakaribisha sana kufungua akaunti zao za NBC Shambani ili wawe kwenye nafasi ya kushinda zawadi hizi zikiwemo pikipiki na laptop,’’ Alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima wenzao, Bw Bakari Salumu na Bi Hawa Rashidi waliwahimiza wakulima wenzao kutoka mikoa hiyo miwili kutumia vema ujio wa kampeni hiyo kujinufaisha kupitia fursa mbalimbali zinazoambatana na kampeni hiyo ikiwemo zawadi, elimu ya fedha, mikopo na huduma nyingine ikiwemo bima za afya na mazao.
No comments:
Post a Comment