Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 14 March 2018

RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA SGR - KUTOKA MOROGORO HADI MAKUTUPORA - DODOMA KM 422 KATIKA ENEO LA IHUMWA NJE KIDOGO YA MJI WA DODOMA. MACHI 14, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kutoka mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma yenye urefu wa km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma. Wengine katika picha ni Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Pro. Makame Mbarawa, Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Reli TRC Masanja Kadogosa pamoja na viongozi wengine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mfano wa Reli hiyo ya Kisasa mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mfano wa Reli hiyo ya Kisasa mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke wakishuhudia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunga kifuniko mara baada ya kutumbukiza karatasi ya majina ya viongozi mbalimbali waliofanikisha ujenzi huo kama kumbukumbu katika uwekaji wa jiwe la msingi la Reli ya Kisasa(SGR) itakayotoka mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saruji iliyochanganywa na kokoto kwenye jiwe hilo la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa kutoka mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma yenye urefu wa km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.

No comments:

Post a Comment