Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 21 October 2016

WAZIRI MAHIGA AZUNGUMZIA MAADHIMISHO YA MIAKA 71 YA UMOJA WA MATAIFA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mhe. Balozi Dkt. Mahiga, amezungumzia umuhimu wa maadhimisho wa Siku ya Umoja wa Mataifa na faida za Jukwaa la umoja huo kwa maendeleo ya Taifa. Maadhimisho hayo yatafikia kilele tarehe 24 Oktoba, 2016.
Mhe. Waziri akiendelea kuzungumza na waandishi wa habari.
Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) akifuatilia mkutano. Kulia ni Kaimu Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bi. Chansa Kapaya.
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Kaimu Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bi. Chansa Kapaya akizungumza na waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment